Pages

Pages

Saturday, June 22, 2013

Mashindano ya riadha ya Tabora Marathon yaliyopangwa kufanyika yaahirishwa



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MASHINDANO ya Riadha ya Tabora Marathon yaliyopangwa kufanyika leo mjini Tabora, yameahirishwa.
Mshauri wa Ufundi wa Tabora Marathon, Tullo Chambo kushoto akizungumza jambo juu ya mashindano hayo.

Akizungumza jana kwa njia ya simu kutoka Tabora, Mshauri wa Ufundi wa Tabora Marathon, Tullo Chambo, alisema kuahirishwa kwa mashindano hayo kumetokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao.
Alisema baada ya kuahirishwa huko, sasa mbio hizo zitafanyika wiki ijayo endapo mambo yataka sawa.


Chambo alisema japo kila kitu kilikuwa kimekamilika, lakini kati ya vitu vilivyotarajiwa kuwapo katika mashindano hayo, kilichelewa kupatikana, hivyo kulazimika kuahirisha kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mbio hizo zinakuwa na mafanikio makubwa.

“Sisi kama wadau wa riadha tuna mipango ya kuona mashinxdano haya yanakuwa na mvuto mkubwa mkoani Tabora.

“Katika hili naamini hata kuahirisha huko kutakuwa ni sehemu ya kuiweka riadha katika kilele cha mafanikio,” alisema.

Tayari wadau wa mashindano hayo wameshawasili mkoani Tabora kwa ajili ya kuhakikisha kuwa Tabora Marathon yanafanyika kwa mafanikio makubwa mjini humo.

No comments:

Post a Comment