Pages
▼
Pages
▼
Friday, June 14, 2013
Masele Chapombe apata mkong'oto baada ya kumvunja mtu mguu alipomgonga na pikipiki na kutaka kukimbia
Na Mwandishi Wetu, Tanga
MSANII Masele Chapombe Ijumaa ya leo imekuwa ngumu kwake baada ya kupata mkong’oto mzito kutoka kwa wananchi alipomgonga mtembea kwa miguu na kutaka kukimbia, hivyo kutiwa mkononi, kabla ya kutoroshwa ili kumnusuru na kipondo hicho.
Masele Chapombe, pichani
Mwandishi wetu kutoka jijini Tanga alisema kuwa Masele alikuwa kwenye gari na ambapo alimgonga mtu kwa bahati mbaya akiwa kwenye pikipiki na kuamua kukimbia, ila mbele tena aligonga tena hivyo kumfanya ashikwe kwa urahisi.
Mtu aliyogongwa na Masele amedaiwa kuvunjika mguu na kuwahishwa Hospitalini, huku akisema Masele hakulazwa Hospitali baada ya kuzushwa kuwa hali yake ni mbaya baada ya kupata ajali hiyo.
“Ni kweli Masele amepata ajali hapa mkoani Tanga, lakini hana hali mbaya kama wanavyosema watu wengine, hasa wale wanaosema kuwa eti yupo mahuhuti, isipokuwa kuwa aliyemgonga amevunjika mguu na inadaiwa hali yake si nzuri.
“Alipata mshike mshike kidogo kutoka kwa wananchi, hata hivyo alifanikiwa kutoroshwa na wananachi na wadau wake,” alisema mtu aliyeshuhudia ajali hiyo mkoani Tanga.
Masele ni miongoni mwa wasanii wa vichekesho wenye uwezo wa juu, huku akifanikiwa kucheza filamu nyingi zenye kiwango cha kutisha, huku staili yake kubwa iliyomuweka juu ikiwa ni ya kuigiza akiwa amelewa kila wakati.
No comments:
Post a Comment