Pages

Pages

Tuesday, June 18, 2013

Konyagi yafanya semina na waheshimiwa wabunge mjini Dodoma




 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa, akionesha kinywaji cha Afrika Kusini kilichofungwa kwenye viroba kama ambavyo Konyagi inafanya hapa nchini.Vinywaji kama hivyo vipo karibu nchi nyingi Ulimwenguni.



 Meneja wa Masoko wa Konyagi, Joseph Chibehe akielezea jinsi vinywaji vyao vinavyochangia mapato ta serikali.




 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo,Maji na Mifugo, Said Nkumba akichangia mada hiyo kwa kuviasa baadhi ya vyombo vya habari kuacha kuandika habari za kudidimiza viwanda vya haba nchini. Kulia ni Idd Azzan Mbunge wa Kinondoni na Dunstan Kitandula ambaye ni Makamu Mwenyekiti was  Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara.

                               Bidhaa mbalimbali zikiwa zimfungwa kwenye viroba
 


 Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makala, akichangia mada katika semina hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Kassim Majaliwa na Said Nkumba.

 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Dunstan Kitandula akichangia mada hiyo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa (kushoto) akimkabidhi jezi Idd Azzan kwa ajili ya timu ya Bunge iliyocheza na timu ya Konyagi kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma Jumamosi.                  

 Meneja Masoko wa Konyagi, Joseph Chibehe (kushoto) akimkabidhi W. Zuberi  msaada wa vyerehani, ambavyo alivipokea kwa niaba ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika, akisalimiana na timu ya Bunge muda mfupi kabla ya pambano lao na timu ya Konyagi, kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

 George Mkuchika akisalimiana na wachezaji wa timu ya Konyagi
 Wachezaji wa timu ya Bunge wakisalimiana na wachezaji wa Konyagi
 Kikosi cha timu ya Bunge kilichochuana na Konyagi
Kikosi cha timu ya Konyagi kilichomenyana na Timu ya Bunge

No comments:

Post a Comment