Pages

Pages

Monday, June 17, 2013

Hatutamuona tena Langa Kileo, azikwa makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam na kuhuzunisha wengi


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HATIMAE mwili wa marehemu Langa Kileo umezikwa leo saa 10 alasiri na kuacha huzuni kubwa kwa wadau na mashabiki wa muziki wa Hip Hop hapa nchini, akizikwa katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Marehemu Langa Kileo enzi za uhai wake.
Mazishi hayo yaliongozwa na Mchungaji Andulile Mbwile wa Kanisa la Evangelistic Of God, Kawe jijini Dar es Salaam, ambapo pia alitumia muda huo kuwakumbusha wasanii kufuata maadili, sambamba na kuacha utumiaji wa madawa ya kulevya na vitu vingine visivyofaa katika jamii yao.
Marehemu Langa Kileo wakati anaagwa nyumbani kwao Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Wakati taratibu nyingine za mazishi hayo zikiendelea, pembezoni zilionekana sura za wasanii wa muziki wa Hip Hop, akiwapo Joseph Haule, Profesa Jay, Stamina, Roma, Kala Jelemia na wengineo wakiwa na nyuso za huzuni katika msiba huo.

Mchungaji alitumia muda mwingi kuwambusha wasanii na jamii juu ya kumrudia Mungu kwa kuacha vitu vya ovyo, kama vile dawa za kulevya na mengineyo.

“Tutuumie msiba wa kijana wetu Langa kujikumbusha kuwa kifo ni lazima kwa kila mtu maana hakiwezi kukimbiwa, ila tufikie wakati tuone sasa ni muda wa kumrudia Mungu na kuacha yote mabaya pamoja na dawa za kulevya zinazopigiwa kelele kupita kiasi,” alisema.

No comments:

Post a Comment