Pages

Pages

Tuesday, June 25, 2013

Habari zilizotufikia hivi punde, Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chadema, Sugu akamatwa mjini Dodoma

HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu amekamatwa na jeshi la Polisi, mkoani Dodoma.
 

Habari hizo zinasema kuwa kukamatwa kwa Sugu kunatokana na kudaiwa kuandika maneno ya matusi katika mitandao, kwa madai kuwa ambayo hayajathibitishwa na Handeni Kwetu Blog kuwa aliandika maandishi yanayotajwa kuwa yalimuita Waziri Mkuu mpumbavu.

Hata hivyo, kukamatwa kwa mbunge huyo kumeanza kutafsiriwa tofauti miongoni mwa jamii, hasa wananchi wa Mbeya na wanaounga mkono sera za mbunge huyo ambaye pia ni mwimbaji wa Hip Hop.

No comments:

Post a Comment