Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KADA wa Chama Cha Mapinduzi na Diwani wa Kata ya Magomeni,
Bagamoyo mkoani Pwani ambaye pia ni mume wa Khadija Kopa, Jafary Ally anazikwa
leo saa tisa mjini Bagamoyo.
Khadija Kopa akimlilia mumewe jana.
Kwa sasa msiba upo kwa wazazi wake Tandale, lakini muda
mchache ujao watu wataanza kuelekea Bagamoyo kwa ajili ya mazishi. Jana
kulikuwa na mvutano, baada ya baadhi ya watu, wakiwamo viongozi wa CCM kutaka
Ally akazikwe Bagamoyo.
Taarifa zaidi ya mazishi ya mume wa Kopa zitaendelea kukujia
katika blog yako ya Handeni Kwetu.
No comments:
Post a Comment