Pages

Pages

Sunday, June 23, 2013

Chama cha ADC: CUF na CCM wamezidi kupoteza dira, lazima waanguke



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
CHAMA Cha Alliance For Democratic Change (ADC), kimesema kuwa sasa vyama vya CCM na CUF vimeanza kupoteza umaarufu wake katika siasa za Tanzania, hivyo kuna siku vitapotea kusipojulikana na kuwaacha wengine wakifanya vizuri.
Mwenyekiti wa ADC, Said Miraaj katikati akizungumza na waandishi wa habari juu ya siasa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hasa Uchaguzi Mdogo jimbo la Chambani, uliomalizika kwa CUF kushinda na kutetea jimbo lao. Kulia ni Doyo Hassan Doyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo mchana, Mwenyekiti wa ADC, Said Miraaj, alisema kuwa hilo limedhidhirika pia katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chambani, ambapo CUF na mgombea wao Yussuf Salim Hussein walipata ushindi wa jumla ya kura  2708.

Alisema ingawa wao wameshika nafasi ya tatu kwa kupata kura 112 nyuma ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliyopata kura 202, huku washindi ambao ni Chama Cha Wananchi CUF kikipata kura 2708, wakati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakipata kura 12, ila njia yao ni nzuri katika kuelekea wao kufanya vizuri kuliko vyama vingine vya siasa.

"Pemba kuja chama na kufanya vizuri ni ngumu mno, ndio maana hata ndugu zetu Chadema wao licha ya kufanya vizuri katika siasa za Tanzania Bara, lakini kule walipata kura 12 tu.

"Sisi kama ADC tunaamini tutafanya vizuri zaidi, hasa kama wapiga kura wetu wataendelea kutuamini na kutuunga mkono, ukizingatia sisi ndio wasemaji wakuu wa watu wa Zanzibar, baada ya ule muundo wa serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema.

Aidha ACD kimemjia juu Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kulitaka Jeshi la Polisi kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaadhibu watakaokaidi amri zao, katika matukio ya kijamii na kisiasa.

Kauli hiyo si ya kwanza kutolewa na watu mbalimbali, wakiwamo wanasiasa tangu Pinda alipotoa kauli hiyo, akichukulia mfano wa mlipuko wa bomu jijini Arusha na jinsi wananchi walivyoshindwa kutii amri halali ya jeshi la Polisi na kuzua mgogoro mzito, huku wakisaidiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

No comments:

Post a Comment