Pages

Pages

Friday, May 03, 2013

Tunawatakia kheri waandishi wote duniani kwa siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari



Waandishi wa Habari wakiwa kazini

LEO ni siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari. Kwasababu hiyo, Handeni Kwetu blog inawatakia kila la kheri waandishi wote duniani. Mikono yao ni muhimu kwa mustakabali wa Taifa lolote duniani. Naamini siku kama ya leo wataitumia kutafakari changamoto zao.

Waandishi wa habari za michezo, Onesmo Kapinga akifuatilia jambo kwenye kompyuta na Zaituni Kibwana.

Ingawa  waandishi kioo cha jamii, lakini nao kama binadamu wa kawaida kuna mahali wanakosea kwa sababu moja ama nyingine. Pia, licha ya umuhimu wao huo, lakini wengi wao wamekuwa wakiishi maisha ya kawaida.

Baadhi yao wananufaika na majina ambayo hata hivyo hayana tija kwao. Hata hivyo, bado haitakuwa sababu ya kutoheshimu mchango wao. Ni wakati wao sasa kuona kuwa Taifa linahiwahitaji kwa namna moja ama nyingine.
Muandishi wa Habari za Kimataifa wa Gazeti la Mtanzania, Joseph Hiza kulia akiwa na Markus Mpangala, wakifurajia jambo.
Kushoto kwao ni Mhariri wa Makala wa gazeti hilo, Hamisa Maganga akiwa kazini.

Hii ni faida kubwa kwao. Changamoto katika jambo lolote ni matokeo ya kawaida, hivyo bila kukata tama, waandishi wanapaswa kuungana na kufanya kazi kwa nguvu moja. Pia wapo waandishi ambao kwa mtazamo hasi, wanaojiona wao ni bora kuliko wenzao.

Hii inazalisha chuki miongoni mwao na kuwafanya wasiwe wamoja katika kukaa na kutafakari maisha yao kwa ujumla. Huu ni wakati wa kufunga mkanda. Bila hivyo, miaka nenda rudi, waandishi wa habari watakuwa daraja la maisha bora yaw engine huku wao wakifa njaa.

Handeni Kwetu blog inawatakia kheri waandishi wote ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment