Pages

Pages

Tuesday, May 14, 2013

Soya na Bungu Kibaoni wapenya Gambo Cup wilayani Korogwe


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
TIMU mbili za Soya na Bungu Kibaoni wilayani Korogwe mkoani Tanga zimepenya katika hatua ya kwanza ya michuano ya Gambo iliyoanzishwa na Mrisho Gambo wilayani humo.
                Mkuu wa Wilaya Korogwe, Mrisho Gambo
Timu hizo sasa zinasubiri kuingia hatua ya robo fainali kwa kusubiri timu nyingine kwenye makundi manne yaliyowekwa kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mshindi halali anapatikana kwa kupitia michuano hiyo.

Akizungumza kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa Chama Cha Soka wilayani Korogwe, Peter Juma, alisema kuwa ligi yao inaendelea vyema kwa timu za Soya na Bungu Kibaoni kupenya hatua ya kwanza.
Alisema kuwa anaamini kuwa timu nyingine zitaonyesha uwezo wa juu katika kushiriki michuano hiyo yenye mguso katika wilaya ya Korogwe iliyoandaliwa na DC Gambo.

“Sisi kama wasimamizi wa michuano hii ya Gambo Cup tunaamini kuwa lengo ni kuona mashindano yetu yanafanya vyema na kukuza mchezo wa soka wilayani hapa.

“Timu za Soya na Bungu kibaoni zitasubiri timu za makundi mengine na baadaye kushiriki hatua ya robo fainali kwa mtindo wa makundi ambapo ni utaratibu uliowekwa kwa ajili ya kufanikisha mashindano haya ya Gambo Cup wilayani Korogwe,” alisema Juma.

Mashindano hayo ya Gambo Cup yalizinduliwa na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete, ambaye ni mtoto wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

No comments:

Post a Comment