HAYA ni maoni na mtazamo wa mchambuzi wa masuala ya Uchumi na Biashara Albert Nyaluke Sanga aliyotoa katika mahojiano yake na wataalamu wa chuo Tumaini walipomtembelea nyumbani kwake Iringa kwa ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali ya kimaisha.
Albert Nyaluke Sanga, mchambuzi wa biashara na uchumi Tanzania
Mwezi uliopita kuna wataalamu wa masuala ya biashara
kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini walifika ninapoishi kunihoji kwa dodoso la kiutafiti;
lengo likiwa ni kujua.
Je, ni kwa nini watu wa kabila
la Wakinga wanafanikiwa sana kibiashara?" Waliuliza maswali mengi lakini
swali lao kubwa lilikuwa ni hili:
"Unaongeleaje dhana
inayoaminika ya kwamba wakinga
wengi wanafanikiwa kibiashara kwa sababu ya ushirikina?
Majibu yangu kwao kwa swali
hili yalikuwa kama hivi: "Ushirikina upo na unaweza kumfanikisha mtu
kibiashara. Hata hivyo ushirikina upo katika makabila yote Tanzania. Cha kujiuliza
hapa ni hiki:
Kwa nini wakinga wengi
wanaonekana kutumia mwanya huu wa ushirikina kufanikisha biashara zao?' 'Ikiwa
kila kabila kuna ushirikina ni kwa nini makabila mengine yasiutumie ushirikina
wao kutajirika kama inavyosemwa kwa wakinga?'
Bila shaka kuna "KITU CHA
ZIADA" kinachowafanya wakinga wafurukute hata kuamua kutumia mwanya wa
ushirikina maadamu wafanikiwe tofauti na makabila mengine; ambayo licha ya
kuushikilia ushirikina lakini hawautumii kibiashara.
Hii ina maana hata UKIONDOA
USHIRIKINA wanaotuhumiwa nao wakinga; bado wakinga wana nafasi kubwa kufanikiwa
kibiashara kwa sababu ya kile
KITU CHA ZIADA cha
kufurukuta, kupambana na kutorudi nyuma. Niliwaeleza kwa kirefu historia ya
imani za waganga wa Ukingani walivyoanza kutoa huo utajiri; nikawaeleza
mabadiliko ya vizazi vitatu vya wakinga na namna ilivyoleta mapinduzi kiimani
na kibiashara. Baada ya hayo nilihitimisha kwa kuwaeleza hivi:
"Ukiacha issue ya
ushirikina, kuna siri zinazofanya wakinga wafanikiwe sana kibiashara baadhi
yake ni hizi, 1) hawatumii zaidi ya wanachoingiza, 2) wanaheshimu akiba kiasi
kwamba MKINGA yupo tayari kufa na njaa lakini asiguse akiba (inaitwa
ekhefumbato),3) wana nidhamu kubwa mno ya matumizi ndio maana wengi wamebatizwa
jina la "mabahiri" (kupewa hela ya bure bure ama kuhongwa na mkinga
itakubidi ufanye kazi ya ziada sana!!!)
4 Hawa jamaa wanapokuwa kwenye stage ya
utafutaji huwa wanajitenga kabisa na starehe ndio maana wengi hudhaniwa kuwa ni
"washamba" 5) wanasaidiana sana kwa kupeana mitaji na 6 hawana WIVU
KABISA mkinga mwenzao anapoinuka kibiashara.
Albert Sanga ni mchambuzi wa masuala ya biashara na Uchumi.
No comments:
Post a Comment