Pages

Pages

Friday, May 17, 2013

Samahani kwa picha hizi: Polisi mstaafu afanya unyama kwa kumpiga mapanga mtoto wake wa miaka minne

Mtoto wa miaka 4 Devotha Gerlad aliyekatwa mapanga na baba yake,hapa akiwa hospitali kwa huduma aya kwanza. (Picha na Audiface Jackson)
 
 
  
Madaktari wakiwa kazini kuhakikisha wanaokoa maisha ya mtoto huyo.
 
Afande Bwire akiwa hoi wodini huku akiwa amefungwa pingu.
 
Inasikitisha sana  kwa mtoto wa miaka minne kufanyiwa kitendo kibaya na baba yake mzazi
Majukumu ya kuokoa maisha ya mtoto huyo yakisonga kwa kasi.
Afande Bwire akiwa na pingu zake wodini
Mkazi wa kitongoji cha Sango kata ya Nyasubi wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga Samson Bwire (54), ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa kumcharanga mapanga mtoto wake Devotha Gerald (4) kwa sababu za wivu wa kimapenzi.Endelea kupitia mtandao huu ili upate habar zaidi.Tukio hilo limetokea jana jioni nyumbani kwa Bwire baada ya kuanza kugombana na mke wake Happiness (28) Elias huku akiwa amelewa pombe ambapo, mkewe alikimbia kitu kilichosababisha kumgeukia mtoto Devotha na kuanza kumkata mapanga kichwani.

Kwa mujibu wa majirani, kelele zilisikika kutoka kwenye mji huo na kwamba walipoenda walimkuta Bwire akichoma nguo za mke wake, na alipowaona aliingia ndani na kuanza kumkata mapanga mtoto huyo huku akiwa amefunga mlango.

Imefafanuliwa kuwa, baada ya kusikia kelele za mtoto, majirani walianza kuvunja milango huku wakiomba msaada kituo cha Polisi na baada ya Polisi kufika walifanikiwa kumnusuru mtoto akiwa amejeruhiwa vibaya sehemu za kichwani.Majirani kwa hasira walianza kumpiga Bwire ambaye ni askari polisi mstaafu wa cheo cha koplo kwa nia ya kumwua, hali ambayo imelipa jeshi la Polisi kazi ya ziada kumnusuru na kumpakia kwenye gari kwenda kituoni.

Hata hivyo Wakati gari la Polisi likiwa katika mwendo wa kasi eneo la soko la Mkulima, Bwire ameruka kutoka kwenye gari na kuangukia kwenye Lami kitendo kilichomsababishia majeraha makubwa sehemu za usoni.

Mtoto Devotha na baba yake Bwire wote wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa matibabu huku Bwire akiwa Chini ya Ulinzi mkali wa polisi.

No comments:

Post a Comment