Pages

Pages

Tuesday, May 21, 2013

Mashindano ya Uzalendo Cup mbioni kutimua vumbi jijini Dar es Salaam



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Makubi Film Production and Sports Promotions, juzi imetangaza kuendesha mashindano ya Uzalendo Cup yakiwa na lengo la kuwawezesha vijana wanaocheza timu za mitaani kuonesha uwezo wao wa kucheza soka, yakipangwa kuanza kutimua vumbi Mei 23.
Willson Makubi, pichani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Willson Makubi, alisema kuwa pia mashindano hayo yatatumika kuwatafutia wachezaji hawa timu kubwa zinazocheza ligi mbalimbali za kitaifa hapa nchini.

Alisema kuwa mashindano hayo mashindano yatashirikisha jumla ya timu ishirini kutoka kata za Makurumla, Mburahati, Manzese, Mabibo na Ubungo zote za Mjini Dar es Salaam, ambapo zitatoa timu za kushiriki katika mashindano hayo.

“Timu hizo ni zifuatazo ni pamoja na Mti Pesa, Dago, Mburahati United, Pampona, Israel Academia, Mingo,Wazulu, Mabibo Sokoni, Makutano, Midizini Market, Arizona, Mzozo, East Daz, Yakusela, Ranger, Umoja, Darton, Uamsho, Kota Football Club na timu ya Wanafunzi wa Chuo cha Filamu  (TFTC).

“Mashindano hayo yamezindulizwa juzi na Mkuu wa kituo cha Polisi Magomeni, ASP Mwanne Salumu, ambapo katika mazungumzo yake, aliziasa timu shiriki kuonyesha vipaji vyao halisi sambamba na burudani ya mpira wa miguu,” alisema.

Mashindano hayo yanadhaminiwa na Redwood Film Academia, Wendo FaceProduction, Global Publishers, Fleva Fm radio Dodoma.

No comments:

Post a Comment