Pages

Pages

Thursday, May 16, 2013

Katibu Mkuu CCM, Abdulrahman Kinana amlima barua nzito mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa ya kutaka amuombe radhi na kufuta kashfa alizompa kabla ya kumfungulia kesi



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, kwa kupitia wakili wake Eric S.Ng’maryo, wamemataka Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa aombe radhi na kuifuta kashfa aliyoitoa dhidi ya Kinana kwa madai kuwa anahusika na meli zilizokamatwa na meno ya tembo huku pia akiwa ni miongini mwa mafisadi.
                 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa
Kwa mujibu wa Tangazo lililochapishwa kwenye gazeti la kila wiki, Raia Mwema la Jumatano, Mei  15, Toleo namba 296, endapo Msigwa hatafuata masharti ya wakili Ng’amaryo ya kumuomba radhi Kinana, basi atafunguliwa kesi itakayokuwa  na madai makubwa na mengi, sambamba na kubebeshwa mzigo mkubwa wa mamilioni ya shilingi.

Wakili huyo alielezea jinsi Msigwa alivyopotosha umma katika mikutano yake ya kisiasa, sambamba na hutuba yake bungeni, akiwa kama  Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mkutano wa Msigwa inadaiwa kuwa aliufanya Aprili 21, shule ya Msingi Mbugani, wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, ambapo alizungumza mengi ambayo yalisababisha usumbufu mkubwa na kuondoa hadhi ya Katibu huyo wa CCM, Kinana.

Kutoa tangazo hilo na tamko rasmi la wakili wa Kinana ni ishara kuwa moto wa kisiasa umezidi kupamba moto, huku watu wengi wakihusishwa katika kashfa ya usafirishaji wa maliasili za Taifa, jambo linalopingwa na watu wengi.

No comments:

Post a Comment