Pages

Pages

Friday, April 19, 2013

Twanga nayo kupagawisha tamasha la Wasukuma Mei 27 jijini Mwanza



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI kongwe na pendwa ya muziki wa dansi nchini  Tanzania, The African Stars ‘ Twanga Pepeta Internatinal’  inatarajiwa kuporomosha bonge la shoo ndani ya Jiji la Mwanza katika tamasha la  la kihistoria la utamaduni wa Msukuma lililopangwa kufanyika Mei 27.
 
Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka

Akizungumza jana Mtaribu wa tamasha hilo ambayepia ni Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya May Way Entertainment Rose Mwita  alisema bendi iyo itafanya maonesho mawili ambapo baada ya CCM Kirumba siku itakayofuata Mei 28 watakuwa katika mji wa Nansio Ukerewe
katika tamasha la kihistoria la utamaduni wa mkerewe matamasha yote yatafanyika kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka usiku.

Mwita alisema bendi ya Twanga Pepeta imekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii na maendeleo ya vijana kupitia muziki. Hivyo, burudani ya bendi hii na burudani nyinginezo zitakazokuwepo ili kuhamasisha wakazi wa Mwanza na Ukerewe kuhudhuria kwa wingi.
 
Rose alisema, “Tamasha hili linalenga kuhamasisha jamii ya msukum na  mkerewe na makabila mengine kuenzi mila na tamaduni. Vilevile, jamii na familia zilizopo ndani na nje ya mikoa yao zikumbuke nyumbani na kutembelea wazee mara kwa mara pamoja na kuezi mila na utamaduni wa kwao”.
 
Aliongeza kwa kusema kuwa, zaidi ya watu 3,000 na familia zao, wanatarajiwa kuhudhuria kwa wingi katika matamasha hayo  yenye mvuto wa kihistoria huku wakipata fursa ya kusikia historia ya msukuma na mkerewe kwa kina toka kwa wazee wanaotoka sehemu mbalimbali hasa kwenye familia za watemi wa Kisukuma na Wakerewe.

Maonesho mengine yatakayokuwepo ni pamoja na kuona maonyesho ya zana za kale za jadi zilizotumiwa na makabila haya mawili,  kucheza ngoma zote za asili ya msukuma na mkerewe pamoja na vikundi tofauti tofauti vya ngoma za asili na sanaa za makabila mengine vyakula vya aina zote  na vya asili ya msukuma na mkerewe.   Vinywaji vyote vya asili ya msukuma na mkerewe.
 
Mwita alisema pia katika kunogesha tamasha hilo kutakua na  burudani toka kwa wasanii wa kizazi kipya kutoka Dar es Salaam.
 
Vilevile alisema, wamewaalika viongozi wa serikali yetu, viongozi wa dini zote, wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa ndani na nje ya mkoa wa Mwanza, viongozi wa asasi zisizo za kiserikali za serikali na wanafunzi kutoka vyuo na shule mbalimbali katika mkoa wa Mwanza.
 
 Wadhamini wa tamasha hili ni pamoja na Balimi Extra Lager, Safari Lager, Pepsi, Star TV, Redio Free Africa, JB Belmont Hotel, Mwanza Institute, Toyo na La Kairo Investiment.

No comments:

Post a Comment