Pages

Pages

Saturday, April 20, 2013

Tuliza akili yako kwenye mapenzi, ukicheza itakula kwako



MAMBO FULANI MUHIMU
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NASHUKURU kwa dhati wewe mpenzi msomaji wa safu hii unayeendelea kuwa na mimi kila siku kama ya leo, huku ukiendelea kuipitia kona hii inayoelezea mambo ya uhusiano na maisha.
Wawili wapendanao
Hakika wewe ndiye wa kushukuliwa kwa kiasi kikubwa maana umeifanya safu hii iendelee kuwapo katika gazeti pendwa. Baada ya kusema hayo, naomba nikukaribishe Jumamosi ya leo kama kawaida yetu.

Tujadili mambo ya uhusiano kama unavyojua ndio kitu ambacho kinawachanganya wengi vichwa vyao, baada ya kutenda kosa moja katika kipindi cha maisha yake.

Ndugu msomaji wangu, binadamu wengi tunaumizwa kweli na macho yetu ambayo baada ya kuona kitu hutushawishi kuona ni vizuri vinavyopaswa kuwa vyetu na kutulia navyo.

Hata hivyo, si kila kionekacho mbele ya macho yetu ni vizuri. Vingine ni vibaya na haviwezi kutupa furaha kamwe. Vitatusumbua tu. Hivyo kama hapo awali ulikuwa na mpenzi wako, mchumba au mume wako, huna budi kutulia na kuona kinachoita mbele yako si kizuri kama ulichokuwa nacho.

Kwanini nasema hivi? Wapo dada au kaka zetu mwisho wa siku wanalia na kusaga meno kutokana na kucheza katika uhusiano wao. Watu hao licha ya kuwa na wapenzi wazuri wanaoendana nao, lakini wamefanya makosa kwa kulazimisha kutoka nje, kisa kuna mpita njia mmoja alimuona na kumtamani.

Si kumpenda, bali alimtamani, jambo ambalo hakika linasababisha ndoa au uchumba wake kusambaratika. Hili ni jambo la kushangaza kweli na linahitaji kuangaliwa kwa umakini mno.

Vyema mtu akakubali matokeo. Ni vizuri mtu akajua kuwa aliyekuwa naye ndio mzuri na mwenye sifa zote. Makala hii ina husu watu kutulia na kuacha mapepe yao katika mambo ya uhusiano wa kimapenzi.

Nasema haya kwasababu tunakutana nayo sana kwenye jamii yetu. Wapo watu hasa wasichana wamejikuta wakianza moja, tena wakikutana na wanaume wadanganyifu baada ya kutamaniwa kwa dakika chache, yeye akaona jambo jema ni kumuacha mtu wake.

Leo wanalia, maana kule walikoacha au kulazimishwa kuachwa kwa sababu ya kufanya mambo ya ajabu kila siku, wenzao wameshapata ndoa, au uchumba wa kudumu,hivyo kuwaacha njia panda.

Ndio hao wanaojaribu tena kuwasumbua wapenzi wao wa zamani, wakipiga simu kutwa kucha, kutuma barua za mwaliko au kadi za dina, kama njia yao ya kujirudisha kwa mtu wake huyo ambaye hapana shaka nashawishika kusema kuwa alimpenda kwa dhati.

Kwa bahati mbaya, dada huyo anavyofanya hivyo, anaumia zaidi kwa kuona hafanikiwi, hasa kama mwenzake yupo kwenye uhusiano na mtu mwingine na amekolea kuliko alivyokolea kwake.

Je, nini kinachoendelea hapa? Nani mwenye kufaidi mapenzi hapa? Na aliyekosea ni nani kati ya watu hawa wawili? Ndio maana nilisema hapo juu, tuliza akili, kwani mtu akicheza tu ni kosa kubwa.

Mapenzi ni matamani ndio endapo yakikuendea vyema, ila yakienda tofuati matokeo yake ni magumu mno. Watu wengi wanaathirika kisaikolojia kwasababu ya kucheza kidogo kwenye uhusiano wao.

Ni vyema watu tukawa makini, hasa kwa kutulia na wenzi wetu kwa ajili ya kuwaza maisha mengine na sio kuwaza mapenzi kila siku, tena yale yanayochagizwa na wapita njia.
 
Wangapi wanalia kutwa kucha kwa kufanya maamuzi mabaya, aidha kwa kuwaacha waliowapenda na kudanganyika na wapita njia wasiokuwa na mapenzi ya dhati hata dakika moja?

Sema chochote unachotaka kwa kupitia mawasiliano yangu hapa chini.
0712 053949
0753 806087

No comments:

Post a Comment