Pages

Pages

Monday, April 01, 2013

Nyosh, Queen Suzy wazua jambo baada ya kukutwa chochoroni wakizungumza



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS wa Vijana Nyosh El Sadaat, ameibua hisia nzito baada ya kukutwa chochoroni na mnenguaji wake mwenye makeke jukwaani, Queen Suzy wakizungumza bila presha wala soni.
Queen Suzy akiwa na Nyosh Sadaat New Msasani Club jana usiku.
Tukio hilo lilibambwa na kamera yetu ya Handeni Kwetu jana usiku katika onyesho la FM Academia Wazee wa Ngwasuma lililofanyika katika Ukumbi wa New Msasani Club.
Rais wa Vijana, Nyosh El Saadat, alipobambwa na kamera yetu katika onyesho la bendi yao ya FM Academia jana, New Msasani Club.

Katika mazungumzo hayo, Queen Suzy alionyesha umakini mkubwa kujibu maswali ya mdakuzi wetu alipoulizwa alichokuwa anajadili katika giza lile la bosi wake, Nyosh.

“Kwani kuna ubaya gani mimi kuzungumza mahali hapa na Nyosh El Sadaat? Au unataka tuwe tunazungumza nini eneo hili,”? Yalikuwa ni majibu ya Suzy alipokuwa akiulizwa na mwandishi wetu aliyekuwa anawafotoa picha mfululizo bila ya wao kujua.

Nyosh El Sadaat anajiita kama Rais wa Vijana, huku akiongoza kwa majigambo katika bendi hiyo inayofanya vyema katika tasnia ya muziki wa dansi nchini, akisifia safari zake za mara kwa mara katika nchi za Ulaya kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali.

No comments:

Post a Comment