Pages

Pages

Thursday, April 11, 2013

Mussa Kitale awafanyia umafia Dayna na Kala Jeremia



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII wa vichekesho nchini, Mussa Kitale, amewafanyia umafia wasanii wawili wa muziki, Kala Jeremia na Mwanaisha Said Dayna, baada ya kuwalaza chumba kimoja na kitanda kimoja akiwaambia eti anawafundisha namna ya kucheza filamu.
Picha zilizovuja za Dayna na Kala Jeremia wakiwa mkoani Tabora

Hata hivyo, baada ya kufanikiwa kuwapiga picha, alisambaza krip hiyo kwenye baadhi ya mitandao ambapo ilianza kutoa hisia tofauti kwa wadau wa sanaa, wakiamini kuwa wawili hao walikuwa wakifanya ngono katika chumba hicho.

Katika mtandao wa Youtube, watu wengi walikuwa wakiporomosha matusi wakisema kuwa wasanii hao wanataka kutumia ngono kama mbeleko yao ya kuwabeba kisanaa.

Dayna alipoulizwa juu ya tukio hilo la kulala chumba kimoja na Kala Jeremia mkoani Tabora, alisema kuwa hawapo kwenye uhusiano wa kimapenzi, ila Kitale anaandaa filamu ambayo wao watakuwapo kwenye kazi hiyo ya aina yake.

“Ni kweli nasikia mengi mtaani na wengine wanatukana wakisema eti sisi ni wahuni au tupo kwenye mapenzi, ingawa ukweli ni kuwa tupo kwenye filamu zaidi.

“Mimi ni msanii, hivyo kuambiwa nicheze filamu kwangu ni kwepesi zaidi, ndio maana naomba wadau na mashabiki wangu waelewe kuwa sipo kwenye mapenzi na Kala,” alisema.

Hata hivyo Dayna hakuweza wazi ni filamu gani anayocheza na Kala, huku akisema kuwa mwenye uwezo wa kuizungumzia zaidi ni muandaaji mwenyewe Kitale.

No comments:

Post a Comment