Pages

Pages

Sunday, April 21, 2013

Mathew Kiongozi: Hakuna bendi kama Twanga Pepeta


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MDAU mkubwa wa muziki wa dansi nchini, Mathew Kawogo, maarufu kama Mathew Kiongozi, amesema kwamba hakunaa bendi imara na yenye mavitu ya ukweli kuliko Wazee wa Kisigino, The African Stars, Twanga Pepeta.
Mathew Kiongozi
Kiongozi aliyasema hayo katika status yake kwenye mtandao wa kijamii wa facebook na kuchangiwa na watu mbalimbali, akiwamo Mwinjuma Muumini aliyechangia kuwa maneno ya mdau huyo yametokana  na mapenzi ya dhati kwenye bendi hiyo.
Mwimbaji wa Twanga Pepeta, Badi Bakule
Kawogo alisema kuwa bendi imara Tanzania kwa sasa ni Twanga Pepeta, hivyo nyingi zinapiga kelele, jambo ambalo limetokana na uwezo wa wanamuziki wa bendi hiyo iliyokuwa chini ya Mkurugenzi wake Asha Baraka.

Hakuna bendi imara kama Twanga Pepeta, hivyo hizo nyingine zinapiga kelele tu,” alisema Kiongozi, ambaye ni miongoni mwa wadau tishio wa muziki wa dansi nchini.

Licha ya kukabiliwa na changamoto za hapa na pale, lakini Twanga Pepeta ndio bendi yenye wapenzi wengi nchini pamoja na kuwa na shoo nyingi kwa wiki kuanzia Jumatano hadi Jumapili, huku ikiwa na waimbaji mahiri akiwapo Salehe Kupaza Mwana Tanga, Luiza Mbutu, Kalala Junior na wengineo wanaoipaisha Wazee hao wa Kisigino.


No comments:

Post a Comment