Pages

Pages

Monday, April 01, 2013

Fid Q, Stamina wagombania demu Coco Beach


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WASANII wawili wa muziki wa Hip Hop nchini, Farid Qubanda Fid Q na Stamina, jana waliacha vituko katika Ufukwe wa Coco Beach, walipojionyesha dhahiri kuwa ni watu wa vitoto baada ya kujitoa mhanga na kuanza kugombania demu.
 Stamina akifanya mashambulizi kwa ajili ya kumpata demu jukwaani. Ilikuwa balaa.
 Hapa hawa wanafanyiwa usaili ili mmoja wapo atoke na mkali kati ya Fid na Stamina.
 Demu aliyewatoa udenda Fid Q na Stamina akifurahia jukwaani.
 Profesa Jay alikuwapo jukwaani katika tamasha la Vodacom Coco Beach
Afisa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, akiwajibika kwa kupiga picha jukwaani.

Vituko vya wasanii hao wanaotamba katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya vilianza baada ya kupanda jukwaani kuimba katika tamasha la wazi lililoandaliwa na Kampuni ya Simu za Mikononi ya Vodacom Tanzania, kwa ajili ya kufurahia Sikukuu ya Pasaka na wateja wao.

Awali, Stamina ndio alikuwa wa kwanza kupanda stejini kuimba, lakini baadaye Fid Q naye alikwea jukwaani kumpa kampani mkali huyo, jambo ambalo lilianza kuibua hisia za wajamaa hao wanavyopenda watoto, yani wachumba.

"Jamani watu wanasema kuwa sisi hatuwezi kutongoza kama wanavyofanya wale wenzetu, sasa nataka mtupandishie kimwali kikali tuanze kusema nacho ili tuonyeshe kuwa nasisi tunayeweza kupita hata hao wengine wa Bongo Fleva,” alisema Fid Q na kuanza kuleta misuko suko kutokana na mashabiki kuanza kuwafanyia fujo watoto wa kike wakitaka wapande jukwaani.

Hata hivyo, baada ya kupanda wasichana wapatao watatu, mmoja alianza kuimbiwa mistari ya papo kwa papo kwa nia ya kumlainisha, jambo ambalo lilifanikisha kumuangukia Fid Q na kumtia kwapani na kushuka nay echini ya jukwaa.

Hata hivyo, staili hiyo ilikuwa ya kimasiahara tu kwa ajili ya kufurahia siku ya Pasaka, na hata kama aliondoka naye, hakuna ubaya hasa kama wenyewe watakuwa wameridhiana baada ya kuonana katika jukwaa hilo.

Tamasha hilo linaendelea leo katika fukwe hiyo ya Coco Beach ambapo burudani mbalimbali kutoka kwa wakali wa muziki nchini, akiwapo Afande Sele, Mashujaa Music na wengineo wamepangwa kutoa burudani katika tamasha hilo la wateja wa Vodacom.


No comments:

Post a Comment