Pages

Pages

Sunday, April 07, 2013

Dk Mwakyembe awapiga vijembe wanaotaka urais Tanzania 2015



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amewataka Watanzania kuwa makini na wanaopita pembeni pembeni kutaka urais kwa madai kuwa si viongozi bora kwasababu ya kudharau Katiba za Vyama vyao na Katiba ya Tanzania, inayoamini rais wake kwa sasa ni Jakaya Mrisho Kikwete.

Mwakyembe aliyasema hayo jana katika Bonanza la waandishi wa habari lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, huku likidhaminiwa na Kampuni ya Bia TBL.
 Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari jana.
 Ally Choki akionyesha shoo kwa mashabiki wa Extra Bongo
Kaimu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd na Mhariri Mkuu wa Gazeti la Mtanzania, Kulwa Karedia (katikati) akiwa kwenye bonanza la waandishi wa habari jana, Leaders Club.
Simon Malugu, akijiandaa kupata msosi.
 Bloggers FC wakiwa uwanjani jana kwenye bonanza la waandishi wa habari. Kama kawaida, Handeni Kwetu Blog nayo ilikuwapo uwanjani. Chezea wewe.
 Mwandishi na mdau wa Maliasili Tanzania, Asha Bani kushoto, kutoka Tanzania Daima akijimwaga maeneo ya Leaders Club kama alivyokutwa jana.
 Mwandishi wa Star Tv, Halima Kambi, mwenye kitambaa cheupe kichwani akijiachia kwenye bonanza hilo jana.
 
Mhariri wa Michezo gazeti la Mtanzania, Mwani Nyangassa akijiachia katika bonanza la waandishi wa habari jana Leaders Club.
Dk Mwakyembe alisema muda wa kuhangaikia urais kwa sasa bado, badala yake wanaosaka cheo hicho wangesubiri mchakato uanze, ikiwa ni njia nzuri ya kumpa ushirikiano rais aliyopo nchini.

“Wanapokuja huko kwetu wakiwa na nia ya kutaka urais wakati huu, tunapaswa kuwaangalia kwa umakini mno ukizingatia kuwa hilo tu linaonyesha hawafai kuwa na cheo cha urais,” alisema.

Bonanza la waandishi wa habari linalofanyika kila mwaka nchini, kwa mara ya kwanza, waandishi wanaojihusisha na uendeshaji wa bloggers wameshiriki katika michezo mbalimbali.

Shangwe kwa wana bloggers ziliongozwa na mkongwe Issa Michuzi, akihakikisha kuwa furaha kwa vijana wake inapatikana, ambapo pia wamiliki hao walipata nafasi ya kujuana na kupanga kwa pamoja kuwa wakutane walau mara moja kwa mwezi.

Katika hali ya  kufurahisha, blogger ya Handeni Kwetu nayo ilikuwapo katika muunganiko wa wachapakazi wa bloggers, huku ikitumia fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru wote kwa kuiunga mkono tangu kuasisiwa kwake.

No comments:

Post a Comment