Pages

Pages

Friday, March 01, 2013

Wanawake 10 wapanda Mlima Kilimanjaro kuhamasisha usawa wa kijinsia

JUMLA ya wapanda mlima maarufu wanawake wapatao 10, kutoka nchi za Nepal, Afrika kusini na Tanzania wanatarajia kupanda mlima Kilimanjaro leo kupitia geti la Machame kwa lengo la kuhamasisha usawa wa jinsia.
 

Wakiwa wamewahi kufanikiwa kupanda mlima mrefu zaidi duniani, mlima wa Evarest, wanawake saba katika nchi ya Nepal wanaungana na wenzao watatu kutoka afrika akiwemo msanii maarufu wa Tamthilia ya Isidingo, Hlubi Mboya maarufu kwa jina la Nandipha.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wapandaji hao, Mkurugenzi wa shirika la chakula duniani nchini Tanzania (WFP), Richard Ragan amesema kuwa la la elimu, kutokana na mamba za mapema, kuolewa wakiwa wadogo pamoja na changamoto ya kukosa fedha za kumudu mahitaji yao na ndio maana wameamua kuwaunganisha katika kueneza elimu ya usawa na ukombozi wa mwanamke.

Ragan amefafanua kuwa mmoja wa wapandaji kutoka Nepali aliwahi kutoroka nyumbani akiwa na umri wa miaka 14, kukimbia unyanyasaji aliokuwa akifanyiwa na ndugu zake pamoja na shinikizo za kuolewa.


 
Katika msafara huo wapo Watanzania Wawili, Ashura Kayupayupa, ambaye ni mwanaharakati dhidi ya ndoa za mapema na Mwalimu Anna Philipo ambaye ni Mwanaharakati dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia kutoka katika jamii ya Wahadzabe.
Kutoka Nepal ni Shailee Basnet, Pujan Acharya, Nimdoma Sherpa, Pema Diki Sherpa, Chunu Shretha, Asha Kumari Singh na Maya Gurang, pamoja na wapiga picha wawili James Gimbrone na Russ Paraseau.

No comments:

Post a Comment