Pages

Pages

Saturday, March 09, 2013

Uhuru Kenyatta ndio rais mpya Kenya, ambwaga Odinga




Uhuru Kenyatta, Rais mtarajiwa kuanzia leo, atakapotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

Na Mwandishi Wetu, Kenya
HATIMAE Wakenya wameamua kufuta ubishi kwa kuamua wenyewe kumuingiza Ikulu, Uhuru Kenyatta, aliyekuwa anachuana vikali na Raila Odinga kwa kujipatia kura Milioni 6, 173, 433.


Kwa matokeo hayo, Kenyatta amefanikiwa kuingia Ikulu, ingawa mpaka sasa bado Tume Huru ya Uchaguzi haijatangaza rasmi kinyang’anyiro hicho cha Urais nchini hapa.

Kadri muda ulivyokuwa unasonga mbele, mamia ya watu nchini hapa walionekana kutumbea kwa furaha, huku wengineo wakiimba nyimbo za kumpongeza Kenyatta kwa ushindi wake huo.

Baadhi waliohojiwa kwa nyakati tofauti, walionekana pia wakishangilia kwa kuwataka Wakenya wote kudumisha amani na kumpa ushirikiano Kenyatta katika uongozi wake.

Kila pembe ya Kenya leo hapa ni shangwe tupu katika kusubiria kutangazwa kwa rais mpya, baada ya bwana Mwai Kibaki kumaliza muda wake kwa kushuhudia rais anayechukua nafasi yake.

No comments:

Post a Comment