Pages

Pages

Monday, March 11, 2013

Uchawi watikisa wilaya za Korogwe na Handeni



Mrisho Gambo, Mkuu wa wilaya ya Korogwe

Na Mwandishi Wetu, Korogwe
HALI ni mbaya kwa wilaya ya Korogwe na Handeni kutokana na vijana wengi kujiingiza kwenye dhahma ya kuita waganga wa kutoa wachawi, maarufu kama lambalamba bila kufuata utaratibu na kuzua hofu.
Mkuu wa wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu

Leo, katika mji wa Korogwe, polisi wamelazimika kutumia nguvu kubwa kutuliza ghasia kutoka kwa vijana waliokuwa wanapinga mganga wao kukamatwa na kusekwa lupango.

Polisi hao walimkamata mganga huyo baada ya kutoa vitu vinavyodaiwa ni uchawi kutoka kwa mtu anayefanya kazi ya kukatisha tiketi katika stendi ya mabasi ya Korogwe, jina lake linahifadhiwa.

Shuhuda wetu aliyekuwa mjini Korogwe, aliiambia Handeni Kwetu kuwa juhudi za polisi kuzuia mganga huyo asiendelee na kazi yake zimesababisha mgogoro na wananchi.

Hapa Korogwe kuna uchawi sana, lakini kwakuwa serikali haiamini uchawi basi wananchi tunaendelea kutumika vibaya, ndio maana hata hao waliotolewa uchawi huo wanalalamikiwa sana.

Suala hili limewafanya baadhi ya watu washindwe kujuzuia na kuzua mjadala kutoka kwa jeshi la polisi juu ya oparesheni hii ya kutoa uchawi katika maeneo ya mji huu,” alisema mdau huyo.

Juhuzi za kufanya mazungumzo na Kamanda wa Polisi za Wilaya na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mrisho Gambo zinaendelea juu ya sakata hilo linalosumbua kwa wiki kadhaa sasa.

Naye Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kuwa wilaya yake imezidi kukumbwa na suala hilo la lambalamba, katika vijiji mbalimbali.

Tumekubaliana kuwa mgogoro kama huu unapotokea, anakamatwa mganga huyo,” alisema Muhingo.

Katika kijiji cha Komsala, wilayani Handeni mkoani Tanga, lilijitokeza suala hilo Ijumaa iliyopita na kulazimika polisi kuvamia na kuwakamata watu mbalimbali ambao hata hivyo baadaye waliachiwa baada ya zogo hilo kumalizika na shughuli za kijamii kuendelea.


No comments:

Post a Comment