Pages

Pages

Friday, March 29, 2013

Simba waivulia kofia Kagera Sugar kwa kuwatoa kamasi



Kukipiga na Toto African kesho Jumamosi Mwanza

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Simba, umesema licha ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya timu ya Kagera Sugar, ila wachezaji wao wamecheza soka la uhakika, ingawa nafasi ndogo zilizotumiwa na kocha wa Kagera, King Abdallah Kibadeni, zilichangia kuwaua katika mchezo huo.
                            Juma Kaseja
Kibadeni ni kocha na mchezaji aliyewahi kuwika na Simba kwa misimu kadhaa, kabla ya kuhamia pia kuinoa klabu hiyo ambayo kwa sasa ipo chini ya Patrick Liewing na wasaidizi wake, Jamhuri Kihwelo Julio na Moses Basena, raia wa Uganda, aliyewahi pia kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.


Akizungumza kwa njia ya simu wakiwa safarini kutoka Bukoba kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya kucheza na Toto African Jumamosi katika Uwanja wa CCM Kirumba, Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema nafasi ndogo walizopoteza na utaaamu wa Kibadeni vilichangia kuwaua na kupata kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Alisema pamoja na matokeo hayo, lakini kwa sasa wanaelekeza nguvu zao dhidi ya Toto African, wakiamini kuwa watapata matokeo mazuri na kuwafurahisha mashabiki wao katika mchezo huo.

“Kagera Sugar ipo chini ya Kibadeni, kocha mwenye uzoefu na pia anawafahamu vyema wachezaji wote wa Simba kwa sababu alikaa kwenye benchi kwa muda mrefu, hivyo kuna uwezekano alitumia ujanja huo na kuchangia wao kuibuka na ushindi huo dhidi yetu.

“Hata hivyo, kwa sasa hatuangalii matokeo hayo ya kufungwa, bali nguvu zote zipo mbele ya Toto African, ukizingatia kuwa mchezo huu utapigwa keshokutwa (kesho) Jumamosi, katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza, “ alisema Kamwaga.

No comments:

Post a Comment