Pages

Pages

Sunday, March 10, 2013

Extra Bongo kukamua leo Garden Breeze, Magomeni




Nadine, mnenguaji wa Extra Bongo na repa wake Papy Catalogue

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam       
BENDI ya Extra Bongo, leo inafanya shoo ya nguvu katika viwanja vya Garden Breeze, Magomeni, katika bonanza lao la kila Jumapili linalohudhuriwa na mashabiki lukuki wanaokwenda kupata burudani katika sehemu hiyo inayopendwa na wengi kwa sasa.


Extra Bongo, maarufu kama Wazee wa Kizigo ama Next Level, inapanda jukwaani ikiongozwa na Mkurugenzi wake, Ally Choki, akishirikiana na wakali kadhaa katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini, akiwamo Ramadhan Masanja, Banza Stone.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Choki alisema kuwa bonanza lao linapendwa na wengi, jambo linalowasukuma mashabiki wao waende kwa wingi kujipatia burudani za aina yake katika kuhakikisha kuwa wote wanapata burudani za aina yake.

Alisema kila Jumapili, bendi yao inafanya shoo katika viwanja hivyo vya Garden Breeze, huku ikihudhuriwa na watu wengi kutoka shemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam wanaokwenda kupata ladha za Wazee wa Kizigo.

“Extra Bongo ni bendi ya kazi sio ya kupiga porojo, hivyo naomba wadau waendelee kuja kwa wingi katika shoo zetu, ikiwapo ya bonanza la Garden Breeze, ukizingatia kuwa limeandaliwa maalumu ya kwa ajili ya kukutanisha watu wote.

“Kila mmoja anaweza kuingia, maana halina gharama, ukizingatia kuwa tangu tuanze bonanza letu tumekuwa na malengo madhubuti ya kufurahia kazi zetu katika kipindi hiki ambacho kila mmoja anataka kuonyesha makali yake,” alisema Choki.

Garden Breeze ukumbi uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam ndio sehemu inayojaza watu wengi katika burudani za mwisho wa wiki, jambo linalowafanya watu kupata nafasi ya kuburudika na kazi nzuri za Extra Bongo.

No comments:

Post a Comment