Pages

Pages

Wednesday, February 13, 2013

Yanga yenye hasira kuivaa kibonde African Lyon leo



Watatukoma leo hao African Lyon

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MABINGWA wa zamani wa Tanzania Bara, Yanga SC, leo inaingia uwanjani kumenyana na African Lyon, katika mechi iliyopangwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Mbali na Yanga, timu nyingine zinazotarajiwa kupigwa leo ni pamoja na Coastal Union ya Tanga, iliyokaribishwa na Kagera Sugar, katika Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba, Toto African na Polisi Morogoro, Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, JKT Oljoro na Mgambo, Mkwakwani, wakati Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting, wakicheza Uwanja wa Manungu, Turiani, mkoani Morogoro.

Mechi hizo zinaingia katika mvutano wa aina yake, hasa kwa upande wa Yanga, inayoshika usukani mwa ligi hiyo, ambayo kwa sasa imefikisha pointi 33, akifuatiwa na Azam FC, Simba SC na Coastal Union.


Mashabiki wa soka wa Yanga, wanazidi kuipa ugumu mechi hiyo, hasa kwa kutaka kwao timu ishinde na kushika nafasi ya juu zaidi, jambo ambalo hata hivyo litakuwa gumu kwa timu zote mbili.

Hata hivyo, Yanga inaweza kumkosa mchezaji wake, Mbuyi Twite, aliyeumia katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki kati ya timu yake ya Taifa ya Rwanda ilipocheza na Uganda, mjini Kigali.

Pamoja na kukosekana kwa mchezaji huyo, tayari benchi la ufundi linaweza kumtumia beji wake Abdul Juma, atakayewavaa African Lyon, ukiwa ni mchezo wa Ligi ya Tanzania Bara.

Katika mechi zote za leo, tambo mbalimbali zimesikikika, kila mmoja akitangaza kuibuka na ushindi katika mchezo huo kwa ajili ya kujiweka katika nafasi nzuri zaidi kwenye patashika hiyo.

Coastal Union kutoka kwa Wagosi wa Kaya, hawa walienda Mwanza kwa Ndege na kuwavaa Toto African ya jijini humo, juzi walikwenda mjini Bukoba kwa basi, huku wakisema watafia uwanjani.

Hali kazalka Kagera Sugar nao wametangaza kuwachakaza wageni wao wa ligi, Coastal, wakisema watautumia vyema uwanja wao wa nyumbani kwa ajili ya kuwaonyesha soka la uhakika Wagosi wa Kaya.

Kwa upande wa Ruvu Shooting, JKT Oljoro, Toto Afrucan, Mgambo Shooting zote zimepania kutoka na pointi zote tatu katika mechi za leo Jumatano, hivyo kuongeza mvuto na ushindani kwenye mechi hizo.

Katika msimamo wa Ligi hiyo, Yanga SC ina pointi 33, sawa na Azam FC, wakitofautiana mabao ya kufungwa na kushinda, wakati Simba wao wana pointi 28, wakitoka sare mechi mbili za mzunguuko wa pili, huku wakishinda mechi moja dhidi ya African Lyon kwa kuifunga bao 3-1.

No comments:

Post a Comment