Pages

Pages

Wednesday, February 27, 2013




Waziri wa Nishati na Madini Mh. Sospeter Muhongo alipata fursa kuongea na Watanzania waishio Uingereza katika mwaliko rasmi kutoka serikali ya Uingerza. Katika ziara yake nchini Uingereza Mh Sospeter Muhongo ameambatana na Bw. Athanas Macheyeki, Bw. Seleman Hatibu na Bw. Sosthenes Massola.

Mh. Muhongo aliwaeleza Watanzani suala zima la gas na jinsi gani serikali itavyotumia gas hiyo kuleta maendeleo ya nchi. Amesema “serikali itahakikisha kuwa kila kijiji kinapata umeme na mpaka kufikia mwaka 2025 nchi ya Tanzania itaondoka na umasikini”. 

Aliendelea kusema kuwa bila ya umeme hatutoweza kutoa umasikini hivyo wizara yake itatafuta miundo mbinu ya kisasa ili kuwezesha suala zima la matatizo ya umeme linaondoka. Pia amesema wizara yake itaangalia tena ufumo wa Tanesco na kuanzisha idara zingine ambazo zitashirikiana na zitawezesha kutatua matatizo yanayoikabili Tanesco.

Vilevile Mh Muhongo aliwataka wawekezaji wa Kitanzania waweze kuwekeza katika sekta ya nishati na madini.

Habari na Ally Muhdin- London



Mh. Balozi Peter Kallaghe




Mh. Peter Kallaghe akimkaribisha mgeni rasmi Mh. Sosper Muhongo kuongea na watanzania



Mh. Sospeter Muhongo akiongea na watanzania




Mama Balozi Joyce Kallaghe pia alikuwepo




Naibu Balozi Chabaka Kilumanga na watanzania waliohuduria wakifuatilia mkutano kwa makini



Wadau mbali mbali waliohudhuria mkutano huo wakisikiliza kwa makini

No comments:

Post a Comment