Pages

Pages

Thursday, February 14, 2013

UCHAGUZI TFF: Serikali yamtwisha zigo zito Leodgar Tenga


Naibu Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni, Amos Makalla

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla, amemtaka Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), kulimaliza haraka tatizo la mkanganyiko wa TFF katika kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu kabla ya serikali haijaingilia kati.

Makalla aliyasema hayo katika televisheni ya ITV usiku huu, akizungumzia juu ya kuenguliwa kwa aliyekuwa Mgombea wa Urais wa TFF, Jamal Malinzi, sambamba na Michael Richard Wambura.

Akizungumza juu ya hilo, Makalla alisema Tenga anapaswa kuingilia kati haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kuondoa ufumbufu na wingu zito lililojitokeza katika kuelekea kwenye Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Februari 24.

"Naomba Rais Tenga aingilia kati kabla ya serikali haijaingilia kati kwa kuwataja walioingiza mgogoro huo katika mchakato mzima wa Uchaguzi huo wa TFF,” Alisema Makalla.

Kauli ya Makalla ni muendelezo wa sakata hilo kama mdau wa michezo, ambapo leo pia ameendelea kumshauri Tenga juu ya kuelekea kwenye Uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment