Pages

Pages

Thursday, February 07, 2013

Pitia Maoni ya Mdau Hussein Sendaro juu ya Ziara ya RC Tanga, wilayani Handeni



 
Mdau wa Hande Kwetu Blog, Hussein Sendaro

YALIYOJIRI KWENYE MKUTANO WA MKUU WA MKOA WA TANGA KATIKA MJI WA HANDENI

Katika kipindi changu cha mapumziko mafupi hapa nyumbani nimebahatika kuhudhuria kufika katika mkutano wa Ndg Chiku Galawa RC-Tanga uliofanyika katika viwanja vya soko la zamani mjini Handeni tarehe 4/2/13.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa yupo ziarani wilayani Handeni.

Baada ya utambulisho mkuu wa mkoa alitoa nafasi tano kwa kila jinsia ambayo yaligusa sekta za maji, barabara, kilimo, mifugo, afya, ulinzi, umeme n.k na wahusika kutoka wilayani walitakiwa kujibu isipokuwa maswali ya ulinzi na usalama yaliyojibiwa na kamanda wapolisi mkoa RPC Massawe.Na hoja na maswali zilijengwa kama ifuatavyo:


-Tatizo la maji limeendelea kuwa kero na hata masuluhisho yake yamekuwa sio mazuri ikitolewa mfano kisima ambacho RC alikizindua katika soko hilo kuonekana haviwezi kutosheleza mahitaji ya wakazi wa mji huu.

Ingawa mhandisi wa wilaya alijibu hoja hii lakini wananchi hawakuridhika na ndipo zomea zomea ilipoibuka kabla ya mkuu wa mkoa kuingilia kati.

-Ubovu wa viwanja vya soko la zamani, solo la ndani na uwanja wa michezo Azimio (Centre).
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji alijibu maswali mawili ya mwanzo kwa kuahidi ukarabati utaanza kwa kuezeka soko la ndani na kuhusu viwanja vya soko la zamani alisema kumetengwa mliloni 15 na tayari zabuni imetangazwa na ikikamilika muda wowote ukarabati utaanza.

Swali la tatu afisa utamaduni alisema mil 20 zimetengwa kwa ukarabati wa uwanja za tayari umeshafanyika,watu hawakuridhika tena na zomea zomea ikaanza

-Kuvamiwa kwa eneo la shule ya msingi Mshikamano kwa ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya Mji Handeni kwa upande mmoja na gereji kwa upande mwingine.

Afisa elimu (Msingi) alisema kashindwa suala hili ambalo lilileta utata sana na mwisho note ikatoka kuwa limefika kwa mkuu wa wilaya na linashughulikiwa.

-Njaa inayoendelea Handeni, pembejeo za kilimo, Afisa kilimo (Wilaya) alitoa ufafanuzi kuwa tayari chakula cha msaada kimefika na kitauzwa kwa bei ya chini kwa wenye kipato cha chini na bure kwa makundi yasiyojiweza.

Kuhusu msimu wa kilimo na pembejeo alisema serikali imejipanga kuhakikisha zinafika kwa wahusika na kwa wakati.

Upungufu wa madawa,matatizo katika wodi za wazazi na watoto.
Mganga mkuu wa hospitali alitolea ufafanuzi, kuhusu madawa alisema yapo ya kutosha na kusababisha zomezomea kuibuka tena.

Wodi ya wazazi alizungumzia tatizo la upungufu wa wauguzi na chumba kutokutosheleza mahitaji na akasema kuna mpango wa kuiongeza wodi hiyo iwe kubwa zaidi, Maji machafu katika mradi wa HTM.

Tatizo halikuongelewa badala yake watu wakaelezwa namna ya kufanya maji yawe salama kwa kutumia water guard au kuchemsha.

Mawsali mengine ambayo yamekosa majibu ya moja kwa moja ni yale ya fidia za wakazi katika kupisha barabara za Handeni-Mkata na Handeni-Korogwe, pia hofu ya kutokulipwa kwa kupisha barabara ya Afrika Mashariki katika maeneo itakayopita mfano Kilimilang’ombe.

Kuhusu swala la ulinzi na usalama kamanda Massawe aliwaasa wananchi kuwa suala la ulinzi linaanzia kwao wenyewe na kuelezea namna jeshi la polisi lilivyojipanga kukabiliana na aina za uhalifu mbalimbali.

Mkuu wa mkoa ataendelea na ziara yake kwa siku nyingine nne zaidi katika maeneno mbalimbali ya wilaya ya Handeni. Maelezo haya pia mdau aliyaweka kwenye group la face book linalojulikana kama Handeni Kwetu.

No comments:

Post a Comment