Pages

Pages

Saturday, February 23, 2013

Yanga, Azam hapatoshi leo Uwanja wa Taifa

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MABINGWA wa zamani wa Tanzania Bara, Yanga SC, leo itamenyana na timu ya Azam FC, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ukiwa ndio mchezo unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki wa kandanda.

Mechi hiyo ya leo, Yanga atakuwa mwenyeji, huku ukipigwa katika Uwanja wa mpya na wenye kubeba watu wengi, akicheza na timu inayopanda juu kwa kasi ya aina yake katika soka Barani Afrika.

Timu zote zinabanana kileleni kwa kuwa na pointi 36, ingawa Azam imecheza mechi moja zaidi, huku zikitofautiana kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa katika msimamo wan a kila moja ina pointi 36.

Huku timu hizo zikichuana vikali kileleni, lakini pia vinara wa ufungaji kwenye ligi kwa sasa wanatoka katika timu hizo mbili, Kipre Tchetche aliyepachika mabao tisa akifuatiwa na Didier Kavumbagu wa Yanga mwenye mabao nane.

Iwapo timu yoyote itafanikiwa kuondoka na pointi tatu katika mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam, kasi ya mbio za kuwania ubingwa itaongezeka.

Waamuzi wanaotajwa kuchezesha mechi hiyo ni pamoja na Hamis Chang’walu wa Dar es Salaam na John Kanyenye wa Mbeya, wakati mezani atakuwepo Oden Mbaga.

Mbali na Yanga na Azam, mechi nyingine zinazopigwa leo ni pamoja na Mgambo Shooting dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, wakati Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi zote za leo zina upinzani wa aina yake, kutokana na timu zote kupania kushinda ili zijiweke katika nafasi nzuri, hasa zile zinazowania ubingwa huo, ikiwamo Yanga, Azam na Simba.

No comments:

Post a Comment