Pages

Pages

Sunday, February 24, 2013

Ni kauli zenya raha na karaha kwa wakati mmoja


MAMBO FULANI MUHIMU
Diamond akiwa na mpenzi wake mpya, VJ Penny

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NATUMIA fursa hii kukushukuru wewe unayependa kuifuatilia kona hii ya 'Mambo Fulani Muhimu', ikiwa na lengo mahususi la kuchambua na kuelezea mada za uhusiano wa kimapenzi.

Ni katika hilo, namimi najikuta nikipata hamu zaidi ya kuendelea kuwa katika kona hii, sambamba na wewe ili kupeana hili na lile.
Hakika, katika hilo, naamini tutaendelea kuwa pamoja kwa ajili ya kuelezama mambo hayo.

Ndugu msomaji wangu mpendwa, wapo watu hasa wanawake hawapendi kujishughulisha.           Ni wavivu kiasi cha kuwakera waume zao.


Ni pale wanapoombwa na waume zao, wawape haki ya ndoa, huku wao wakiwawekea ngumu. Hawataki kabisa kwa kisingizio kwamba wamechoka.
Wengine husingizia usingizi, wakitaka walale kwanza hadi watakapoamka. Hali hiyo ni mbaya sana. Maana wanaume ndio huwaumiza zaidi.

Wao wanapotaka haki hiyo ya ndoa, huwa wameshafika hisia, jambo ambalo kwakweli ni gumu. Kwa bahati mbaya, akina mama hao wanaosema kwanza walale, hawawezi kuamka wenyewe hadi watakaposumbuliwa upya.

Hii ni mbaya kwakweli. Inawatesa na kuwasononesha wenzao, ndio maana baadhi yao huchoka hivyo kuamua suluhisho pekee ni kuwa na wapita njia.
Wale ambao hawataki waambiwe, maana wanajua fika njia ya kwanza ya kumteka mwanamume ni kumlaghai, kumpa raha ya ndoa hadi achanganyikiwe.

Nafikiri hili ni jambo ambalo tunatakiwa tuliangalie upya katika hali ya kuboresha ndoa zetu ama uhusiano wetu. Jua kabisa mikono yako ndio inayoweza kuvunja ndoa yako ama uhusiano wako kwa mwenzako.

Huna budi kuwa makini kwa nia ya kuhakikisha kwamba ndoa yako inaendelea kuchanua na sio kusambaratika kwa ujinga wako unaosumbuliwa na uvivu.

Baadhi yao hujikuta wakisema, “nimechoka bwana ngoja kwanza nilale hadi nitakapoamka,” Kauli hii ni nzuri kwao, ila ni mbaya kwa wenzao.

Hasa inapotolewa kila siku, kama njia ya kumnyima mwenzake haki ya ndoa. Nasema haki ya ndoa kwa wale waliobarikiwa na Mungu juu ya jambo hilo.

Wanamume hao wanachukizwa na mambo hayo, wakisema yanawaumiza wao, hasa wanapohitaji haki yao, ukizingatia kwamba hata dini imeruhusu.

Sawa, dini imeruhusu kwa wale walioingia kwenye ndoa, hivyo sidhani kama yupo mwanamke ambaye anaweza kukataa tu ali mradi amkomowe mume wake.

Hiyo siyo tabia nzuri hata kidogo. Mnapokerwa na tabia mbaya ya uhuni wa wanamume wenu, pia mcheze kwenye nafasi zenu kwa kuziba ufa huo wa umalaya.

Mwanamume asiyetosheka kwa mke wake, hakika ana nafasi kubwa kutoka nje ya ndoa. Huo ndio ukweli. Wewe ambaye hii ni tabia yako kuwa makini.

Unapaswa kujua kiasi gani mtu wako anahitaji dozi zako, ndio maana ameamua kuwa na wewe. Na kama hutaki tena, mpe sababu za kueleweka, lakini sio usingizi.

Huo ni umbea. Usingizi unakujaje katika dimbwi hilo la mahabati. Acha hizo wewe. Nani anaweza kusinzisia hapo? Labda wewe, lakini mwenzako hawezi kulala, eti kwasababu wewe umemwambia ulale kwanza.

Yeye atalala macho. Akikusubiria uinuke ili umpe haki yake ya ndoa. Wasi wasi ni kwamba kuna siku utainuka, wakati yeye ameshawasha gari na kwenda kwa madada poa wanaojiuza ili apumzishe maumivu yake.

Utajisikiaje utakapoletewa magonjwa ya zinaa kwasababu ya ujinga wako? Jiulize mwenyewe, maana hakika wewe ni tunu ndio maana mwanamume wako ameamua kuwa na wewe, hivyo lazima uwe makini.
kambimbwana@yahoo.com
0712 053949
0753 806087

No comments:

Post a Comment