Pages

Pages

Tuesday, February 05, 2013

Ngwasuma kukamua Valentine Day Arcade House



Rais wa Wazee wa Ngwasuma, Nyosh El Sadaat

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, inatarajia kufanya shoo ya aina yake katika Ukumbi wa Arcade House, Mikocheni, katika Sikukuu ya Wapendanao (Valentine Day), inayoadhimishwa duniani kote kila Februari 14.

Akizungumza  na Handeni Kwetu, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa bendi hiyo, Kelvin Mkinga, alisema kwamba shoo hiyo itakuwa ya aina yake kwa kupania kuwapa raha wapendanao.

Alisema kuwa shoo hiyo itadhaminiwa na kupambwa na shangwe za kinywaji cha (Windhoek), inayotumia ukumbi huo kwa ajili ya kuwapatia mashabiki burudani kali ya muziki wa dansi.

Mkinga alisema kuwa shoo yao ni muhimu huku ikifanyika Siku ya Wapendanao na wadhamini wakiwa ni kinywaji cha Windhoek, wakipanga kutoa zawadi mbalimbali kwa wadau na mashabiki wao.

“Itakuwa ni shoo ya aina yake katika ukumbi ule, hivyo naomba wadau na mashabiki wetu waje kwa wingi kupata ladha kamili kutoka kwa waimbaji wenye mvuto mkubwa, akiwamo Patchou Mwamba ‘Tajiri’.

“Huwa hatubabaishi katika shoo zetu, ndio maana wadau wote wanajua kuwa Ngwasuma hakuna zaidi katika tasnia ya muziki wa dansi nchini, ukizingatia kuwa shoo yetu na nyimbo zetu ni moto wa kuotea mbali,” alisema Mkinga.

Nyimbo za Ngwasuma zinazofanya vyema katika kona ya muziki wa dansi nchini ni pamoja na Otilia, Heshima kwa Mwanamke, Vuta Nikuvute na nyinginginezo, wakiwa chini ya Rais wao, Nyosh El Sadaat.

No comments:

Post a Comment