Pages

Pages

Sunday, February 10, 2013

DRFA kuzisaidia kiuchumi timu zake Ilala


Mpira ni pesa, jambo linalowafanya wachezaji wengi duniani kuishi kitajiri kwa kazi hiyo uwanjani.
 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CHAMA Cha Mpira wa Miguu mkoa wa Dar es Salaam (DRFA),
kimeahidi kuzisaidia kiuchumi timu zote za mkoa wa Dar es
Salaam zitakazofikia hatua ya kuuwakilisha mkoa katika
mashindano mbalimbali.

Mwenyekiti wa DRFA, Almasi Kassongo alibainisha hayo jana, wakati
akizungumzia kuwapo kwa kilio cha muda mrefu kwa timu za mkoa huo, kwa DRFA kutozisaidia timu hizo zinapokuwa katika hatua za uwakilishi wa mkoa.

"Malalamiko haya nimeyasikia tu sana, na tumetafuta njia
mbadala, tutakuwa tukisaidia timu zikifika katika hatua ya
uwakilishi, lakini kuzisaidia timu katika maandalizi ya chini,ni
jukumu la DRFA kuhakikisha timu zinapata maendeleo.

"Timu zikiwa nyingi na zikipata mafanikio ndiyo mwanzo wa
kipato chetu, kwa hiyo ni lazima tuzisaidie timu zetu, hali
kadhalika ni jukumu letu tunapandisha viwango vya makocha
pamoja na waamuzi," alisema Kassongo.

Hata hivyo alisema changamoto walizonazo ni nyingi katika
kuendeleza mpira wa miguu nchini, hivyo wamejipanga vizuri
katika kuzitatua na kuwataka wadau wa mpira wa kuwapa muda
katika kuyatafutia ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment