Pages

Pages

Wednesday, February 13, 2013

Ally Choki kumtambulisha upya Muumini Machi Mosi


Mkurugenz wa Extra Bongo, Ally Choki

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya Extra Bongo, Next Level, imepangwa kuusindikiza utambulisho wa bendi mpya ya Victoria Sound, unaotarajiwa kufanyika Machi Mosi, katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni.
Mwinjuma Muumini, Rais wa bendi ya Victoria Sound

Utambulisho huo unakuja siku chache baada ya Mwinjuma Muumini, Rais wa bendi ya Victoria Sound, kuisuka upya kwa kuwaunganisha waimbaji wenye uwezo wa juu, akiwamo Waziri Sonyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Victoria Sound, Hamis Mahelo, alisema kwamba mpango wa utambulisho huo upo sawa kwa ajili ya kuwatambulisha moja kwa moja wakali wao.

Alisema wanamuziki wao wapo kwenye kiwango cha juu katika kuwapatia burudani wapenzi wao, wakiwa pamoja na Extra Bongo, akiwa sambamba na bendi yake ya Extra Bongo.

“Naomba mashabiki waje kwa wingi katika utambulisho wetu huo ambao naamini ni mwanzo mzuri kwa upande wa muziki wa dansi hapa nchini, ukizingatia kwamba ndio tunaingia rasmi.

“Naamini kila kitu kitakuwa sawa, kwa kuhakikisha maandalizi yetu kabambe, tukiwa chini ya Muumini, akiwa ni mwanamuziki mwenye makali ya hali ya juu katika muziki wa dansi,” alisema.

Victoria Sound, tayari imeshaandaa nyimbo kadhaa, ukiwamo ule wa Shamba la Bibi, unaodaiwa kuwa kijembe cha Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka.

No comments:

Post a Comment