Kikosi cha Yanga
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MABINGWA
wa zamani wa Tanzania Bara, Yanga SC, leo imewaangushia kipigo cha mbwa mwizi
wageni wao, timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini, baada ya kuwatandika mabao
3-2.
Mabao
ya Yanga yalipatikana katika dakika ya 32 lililowekwa kimiani kwa njia ya
penati na Jerryson Tegete, Frank Domayo dakika ya 63, kabla ya 72 Tegete
alipoongeza kalamu ya mabao kwa kuandika bao la tatu.
Mabao
ya Black Leopards yalipatikana katika dakika ya 46 lililofungwa na Hampherey
Khoza, huku lile la pili likifungwa na Rodney Ramagaleki katika dakika ya 88,
hivyo matokeo kuwa bao 3-2.
Mchezo
huo ulikuwa na ushindani wa aina yake, kutokana na timu zote mbili kukamiana
kwa ajili ya kuipatia ushindi, ila Yanga wao walikuwa juu zaidi na kufanikiwa
kuibuka na ushindi huo mnono.
Mchezo
huo ni wa Kimataifa wa kirafiki uliowakutani katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar
es Salaam, ukiwa ni mchezo mahususi kwa ajili ya kuwapima wachezaji wa Jangwani
waliokuwa kambi ya wiki mbili nchini Uturuki.
Pia
mchezo huo ni sehemu ya maandalizi kwa timu ya Yanga inayojiandaa na mzunguuko
wa pili wa Ligi ya Tanzania Bara, huku wao wakiwa kileleni.
No comments:
Post a Comment