Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura
Na Mwandishi Wetu, Dar
es Salaam
TIMU ya Yanga na Tanzania Prisons zimeingiza
mapato ya jumla ya sh. 101,016,000 katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom
kuwania ubingwa wa Tanzania Bara iliyofanyika jana (Januari 28 mwaka huu).
Mechi hiyo namba 94
ilichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao
3-1. Watazamaji 17,946 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio
vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Watazamaji 16,158 kati
ya hao walikata tiketi za sh. 5,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ni
98 waliokata tiketi za sh. 20,000.
Kila klabu imepata mgawo
wa sh. 24,314,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
15,409,220.34. Asilimia 15 iliyokwenda kwenye uwanja baada ya kuondoa VAT na
gharama za tiketi ni sh. 12,363,433.45.
Mgawo mwingine wa mapato
hayo ni tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 7,413,060.07, Kamati ya Ligi
sh. 7,418,060.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,709,030.03
na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,884,801.14.
No comments:
Post a Comment