Pages

Pages

Monday, January 07, 2013

Yanga kuvaana na Denizlisport kesho Uturuki

 Na Baraka Kizuguto, Uturuki
MABINGWA wa zamani wa Tanzania Bara, Yanga SC, kesho inajitupa katika Uwanja wa Selen Football kwa ajili ya kupepetana na timu ya Denizlisport ya nchini Uturuki.

Taarifa iliyotumwa na kutoka Uturuki zinasema Yanga iliyoweka kambi ya mafunzo jijini Antalya, nchini Uturuki, itatumia mchezo huo kama njia ya kujipima nguvu na timu hiyo la Denizlispor FC iliyoshuka daraja, ikitokea ligi kuu ya nchi hiyo.

Kocha wa Yanga, Ernest Brandts, pichani, amesema kupata mechi kubwa kama hiyo ni nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Denizlispor FC yenye wachezaji wa kiwango cha kimataifa.

Alisema baada ya kuwa na wiki moja ya mazoezi na mechi moja ya kirafiki dhidi ya Armini Bielefeld ya Ujerumani mwishoni mwa wiki, itakuwa ni fursa nyingine ya kucheza mchezo mwingine kwa ajili ya kujiweka sawa zaidi.

No comments:

Post a Comment