Pages

Pages

Thursday, January 03, 2013

Waziri wa JK achangia laki mbili msiba wa Sajuki




Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dkt. Makongoro Mahanga, akizungumza msibani jioni ya leo, Tabata Bima. Kulia kwake ni Steve Nyerere wakati mwenye suti nyeusi ni Idd Azzan anayeuguza mkono wake.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Kazi na Ajira ambaye pia ni mbunge wa Segerea, Dkt. Makongoro Mahanga, ametoa laki mbili kama rambirambi yake katika msiba wa msanii Juma Kilowoko, Sajuki, nyumbani kwake Tabata Bima, leo jioni.

Kitale rais wa mateja kushoto akiranda randa katika msiba wa Sajuki leo.

Mbali na Mahanga, wengine waliotoa rambirambi zao leo ni pamoja na Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan, aliyetoa laki tano, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba, aliyetoa Sh 1,000,000, Meya wa Ilala, Jery Slaa aliyetoa Sh 1,000,000, katika msiba unaohitaji fedha zisizopungua milioni nane.

Msanii Dokii kushoto, akisikiliza maongezi ya mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan katikati na msanii Masanja Mkandamizaji mwenye miwani, A.K.A Nikikukera, livumini aloniiiiiiii.

Katika maneno yake kwa waombolezaji, Mahanga aliwataka Watanzania kumuombea Sajuki kutokana na msiba wake kuwa pigo kubwa katika tasnia ya sanaa sanaa hapa nchini.

Alisema kifo cha Sajuki ni pigo, hivyo akiwa kama Mtanzania, Mbunge wa alipofia msanii huyo, ameumia vikali na kuahidi kuwa karibu na wote kwenye msiba huo.

“Nimeumia kupita kiasi na hakika msiba huu umekuja katika kipindi ambacho ni kigumu mno kwetu, hivyo naahidi kuwa karibu katika shughuli hizi za kumhifadhi kijana mwenzetu, Sajuki,” alisema.

Azzan yeye alitumia muda mwingi kumuombea dua njema Sajuki, huku akisema anashukuru kuona msanii huyo ni mwenye kujua shukrani, hasa alipowashukuru Watanzania kwa kumchangia.

Wengine waliotoa rambirambi hizo ni pamoja na Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, aliyetoa Sh laki tano, huku msanii Steve Nyerere, akiwashukuru wote kwa michango yao na kusema hadi sasa wamebakiwa na pengo la Sh milioni tatu.

“Tuna pengo la Milioni tatu baada ya wadau wote kutoa na kufikia Sh 5,000,000 ambapo kwakweli wakati tunaendelea kuwaomba wenzetu, waliotoa wote tunawashukuru kwa kushiriki kuwa na sisi,” alisema.

Watu wengi walikutwa katika nyumba ya marehemu Sajuki kwa ajili ya kuomboleza msiba huo kwa ajili ya mpendwa wao anayezikwa kesho saa tano asubuhi, katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment