Pages

Pages

Sunday, January 06, 2013

Wastara amwagiwa sifa kwa kumtunza Sajuki


Sajuki enzi za uhai wake akiwa na mke wake, kipenzi chake, Wastara

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WADAU wa sanaa hapa nchini, wameendelea kummwagia sifa mwanadada Wastara Juma, aliyekuwa mke wa marehemu Sadiki Juma Kilowoko, maarufu kama Sajuki kuwa ana moyo wa aina yake.

Hiyo imetokana na historia ya uhusiano wake na Sajuki hadi kufunga ndoa kukumbwa na mitihan mingi, jambo ambaloh hivyo halikumfanya ajiweke kando na Sajuki.

Akizungumza na Handeni Kwetu, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe, alisema kwamba Wastara ana mapenzi ya dhati na anastahili sifa.

Alisema ameweza kumuuguza mumewe mwanzo hadi mwisho wa uhai wake, jambo ambalo limekuwa gumu kwa baadhi ya watu, kadri muda unavyozidi kwenda mbele.

"Ni mfano wa kuigwa kwakweli kutokana na historian a matatizo mengi yaliyowakumba yeye na mumewe hadi kufariki na kuzikwa Ijumaa katika makaburi ya Kisutu," alisema.

Naye Mbunge wa Kinondoni, kwa tiketi ya (CCM), Idd Azzan, alisema amekuwa karibu na sanaa kiasi cha kumuona Wastara ni miongoni mwa wanawake makini.

"Kwa dunia ya leo kumuuguza mume wako katika kipindi kigumu cha ugonjwa wake, hadi kuchangiwa fedha za kumpeleka India, hakika baadhi yao wanaweza kuleta wasiwasi kidogo,” alisema Azzan.

Azzan ni miongoni mwa wabunge wanaofuatilia sanaa kwa karibu zaidi, huku wasanii wengi wakikimbilia kwake kila wanapokuwa na jambo linalohusu msaada kutoka kwa jamii nzima.

No comments:

Post a Comment