Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Khamis Juma
Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
JUMUIYA
za vyama vya siasa ni muhimu sana.
Jumuiya ndio muhimili wa chama chochote cha siasa. Kwa Tanzania, jumuiya za
chama, kikiwamo Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimekuwa na ukakasi sana.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mboni MhitaLicha ya kuwa na purukushani nyingi katika utafutwaji wa viongozi wake, lakini baada ya kupatikana, umuhimu wake hauonekani. Wote huwa kimya, wakishindwa kukitetea chama.
Nasema
haya huku nikiangalia namna jumuiya ya Umoja wa Vijana CCM (UVCCM),
wanaposhindwa kutangaza vipaumbele vyao katika kuhakikisha kuwa chama kinakuwa
salama.
Katika
Uchaguzi uliofanyika mjini Dodoma
mwaka jana, tulishuhudia vijana wakitunishiana misuri wakishinikiza au kutetea
baadhi ya watu wao ambao kwa kiasi fulani walishindwa.
Ingawa
mwenyekiti Taifa alibahatika kuchaguliwa Sadifa Khamis Juma, kuna uwezekano
mkubwa kuwa atashindwa kuimudu kasi ya kisiasa inavyozidi kuwa juu siku hadi
siku.
Huku
Sadifa akishinda nafasi ya uenyekiti katika uchaguzi huo, Makamu Mwenyekiti
alichaguliwa Mboni Mhita, mtu ambaye kwa pamoja baadhi ya vijana walipinga na
kusema ushindi wao ulitawaliwa na hira.
Sitaki
kusema zaidi juu ya ushindi wa wanachama hao wa CCM, ila kikubwa ni kujadili
namna gani jumuiya hiyo inaweza kujiendesha kwa kushindana na kasi ya
mabadiliko ya kisiasa.
Watu
wengi wamekuwa na mawazo kuwa CCM imezeeka na inastahili kuwekwa kando ili
kupatikana chama mbadala wa kuliongoza Taifa.
Ni mawazo
yanayoweza kuaminiwa na wengi, maana kupanuka kwa sekta ya mawasiliano, habari
mbaya za CCM zimekuwa zikisambazwa kwa njia mbalimbali.
Kwa
mfano, unaweza kufungua email na kukutana na ujumbe unaoeneza sumu mbaya ya
kushindwa kwa CCM kuwaongoza Watanzania. Mbali na hilo, kwenye mitandao ya kijamii habari hizo
sasa ni kawaida.
Kwa
bahati mbaya, sumu hiyo inasambazwa zaidi kwa vijana, wakiamini ndio wenye
uwezo wa kufanya mabadiliko. Wanajua kama vijana wakiamua, basi malengo
yatatimia.
Kwa
wanaofuatilia siasa za Tanzania,
watakubaliana na mimi kuwa, siasa zinazofanywa na vyama vya upinzani
zisipoangaliwa, hali inaweza kuwa mbaya kwa chama tawala.
Vyama
hivyo vimekuwa vikifanya kazi kubwa ya kueneza elimu ya uraia ambayo ndio
tatizo kubwa. Kama hivyo ndivyo, basi kuna
sababu sasa jumuiya za CCM, hasa ya vijana kubuni namna gani ya kuwatembelea
wanachama wao kueneza sera na ilani za chama chao.
Wao kama
jumuiya inayojipambua ya vijana wana kila sababu ya kuwaweka sawa vijana
wanaoyumbishwa na sakata la urais 2015. Baadhi yao wanatumiwa ovyo ovyo na wanasiasa bila huruma.
Wengine
wamemwagwa katika mitandao ya kijamii wakihubiri hili na lile kwa ajili ya watu
wao. Kwa bahati mbaya, watu hao wanapofanya kazi hiyo hawaangalii athari ya
chama chao.
Kwa
mfano, mtu yupo tayari kumtukana au kumsema kiongozi fulani kwa ajili ya
kumbeba yule amtakae. Hii sio njia nzuri.
Sote
tunaamini kuwa kampeni bado na kinachofanywa sasa ni hisia na maandalizi ya
kiundani, maana hakuna mwanasiasa hata mmoja ndani ya CCM aliyetangaza
hadharani kuwa anagombea urais 2015 akipitishwa na chama chake.
Kwa
sababu hiyo basi, huyu Juma na Mboni na viongozi wengine wa jumuiya hiyo ya
UVCCM wanafanya nini kunusuru msururu huu wa vijana wanaoweweseka na siasa za
maji taka?
Wao kama
viongozi wa vijana wote wa Tanzania
waliokuwapo ndani ya chama hicho kikongwe, wamefanya ziara ngapi kwa ajili ya
kutafuta wanachama wapya na kuwaweka sawa wale wanaotaka kukihama, au wale
wanaolia na maisha duni kutoka kwenye serikali ya CCM?
Wao kama
jumuiya ya vijana, inafanya kazi zake kwa mtindo gani kuhakikisha kuwa wote
wanakuwa kitu kimoja? Je, yale makundi yaliyoundwa katika kipindi cha uchaguzi
yamevunjwa?
Kama hayajavunjwa, hawaoni athari kwa CCM itazidi kuwa kubwa
na kuyumbishwa katika Uchaguzi ujao, ukiwamo wa Serikali za Mitaa? Maswali kama
haya majibu yake ni njia nzuri kwa uhai wa CCM.
Tuachane
na wale wanaosema chama kinapendwa. Ndio kinapendwa, lakini si wote
wanaokipenda na kukiheshimu. Chama kitapendwa zaidi kwa kuhakikisha waliokuwa
kwenye uongozi wanafanya kazi nzuri na kuondoa kero za Watanzania wao.
Kama jumuiya zitafanya kazi kwenye uchaguzi wa ndani tu, chama
kitaanguka. Huo ndio ukweli wa mambo. Wanachama wa CCM wanastahili kulijua hilo kwa ajili ya uhai wa
chama chao.
Mara
baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akirithi mikoba
ya Willson Mukama, alifanya ziara katika baadhi ya mikoa kufanya mikutano ya
hadhara.
Pamoja na
mambo mengine, Kinana alitumia nafasi hiyo kuwazindua watendaji wa serikali
ambao wapo chini ya CCM, wakiwamo mawaziri ambao baadhi yao walikuwapo na kujibu maswali ya wananchi
wao.
Ni hatua
nzuri sana kwa
ajili ya kutangaza sera, kutafuta wanachama wapya, maana bila hivyo hali
itakuwa mbaya. Ni kweli, hivyo nilitegemea kuwa hata hizi jumuiya za CCM,
ikiwapo ya UVCCM, wanaweza kutumia njia hiyo, ukizingatia kuwa ni wenye nguvu
zao.
Badala ya
kumsubiri Kinana aende huku na kule kuelezea sera za chama chake, Juma na
viongozi wenzake wanatakiwa waifanye wao kazi hiyo kwa kutembelea sehemu hizo
kuzungumza na wapiga kura wao.
Naamini
katika ziara hiyo, faida yake kubwa ni kuona inawavutia vijana ili waingie kwa
waliokuwa nje au kuwazuia waliokuwa ndani wasitoke na kuhamia kwenye vyama vya
upinzani.
Sitaki
kuamini kuwa ni kweli viongozi waliochaguliwa katika jumuiya ya UVCCM hautakuwa
na jipya na kutekwa kabisa na jumuiya nyingine.
Ukiangalia
kwa haraka, utagundua jumuiya ya vijana CCM ina nguvu kwenye uchaguzi maana
joto hilo hukolezwa na wenye mlengo wao wa
kisiasa, huku wengineo wakimwaga ‘noti’ kama
ilivyodaiwa na wahusika.
Lakini kiutendaji
na kuvitetea vyama vyao, nashawishika kusema kuwa, viongozi wa hao wa upinzani
wamekuwa juu mno. Hii ni picha mbaya. Picha isiyovutia kwa Tanzania yenye
kelele za mabadiliko.
Kupoa
huku kwa jumuiya za CCM, hasa UVCCM ni dalili njema? Wao kama wamelala kiasi
hiki, je, ni kijana gani anayetaka kuwa mwanachama atakuwa kwenye kundi lao?
Kuna haja
ya kuinuka kwa viongozi hao wa UVCCM. Kuna hatari kubwa kwa kukaa kwao kimya,
hasa kwa waliokuwa wakipayuka kulia na ushindi wao kupata la kusema kuwaaminisha
Watanzania kuwa waliochaguliwa hawakuwa na jipya, hata la kuwaunganisha vijana
ili wazungumze kitu kimoja kinachohusu Tanzania na chama chao.
Kulisema
hili kunahitaji moyo wa chuma, hasa kwa wale ambao daima wamekuwa makini
kusubiri kusifiwa na sio kukosolewa, jambo ambalo katika Dunia ya leo halipo.
Natuamini
baada ya kusema haya, Juma na Mboni wao kama viongozi wa umoja huo wa vijana wa
CCM watakaa na kutafuta namna ya kusaidiana na viongozi wengine wa CCM, akiwamo
mwenyekiti wao, Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Vijana
wakifanya kazi imara za chama, hata wakubwa wao hawatakuwa na kazi ngumu ya
kufanya, hasa kitakapofika kipindi cha uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambao kwa
hakika utakuwa na ugumu wa aina yake.
Ni pale
wapinzani, wakiwamo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha
Wananchi (CUF), TLP, NCCR-Mageuzi na vinginevyo vinavyopigania kulikomboa
Taifa, wakisema kuwa CCM kimeshindwa kuwaongoza Watanzania na kuwaletea maisha
bora.
0712
053949
0753
806087
No comments:
Post a Comment