Machael Wambura, mgombea wa Makamu wa Rais TFF
Na Kambi Mbwana, Dar es
Salaam
Kamati ya Uchaguzi ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesema waliowekewa pingamizi na wa
walioweka pingamizi hawaruhusiwi kufika katika kikao cha kesho (Januari 30
mwaka huu) wakiwa na vikundi vya ushangiliaji au wapambe.
Kikao cha kupitia
pingamizi kitafanyika saa 4 asubuhi na wapambe au washabiki wa waombaji uongozi
pamoja na waweka pingamizi hawakiwi kuwepo kwenye eneo la kikao hicho.
Akizungumza leo jijini
Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface
Wambura, alisema wote walioweka pingamizi na waliowekewa pingamizi barua zao za
mwito wa kuhudhuria kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya TFF zimeshatumwa
kwenye anwani za barua-pepe zilizo kwenye taarifa za pingamizi au kwenye fomu
za maombi ya uongozi.
Leo waombaji uongozi
watatumiwa barua za mwito kwa barua-pepe wa kuhudhuria usaili utakaofanyika
tarehe 01-02 Februari 2013. Tarehe 01 Februari 2013 watasailiwa waombaji
uongozi wa TPL Board na waombaji ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kupitia
Kanda ya 1 hadi Kanda ya 8. Waombaji uongozi kupitia Kanda ya 9 hadi ya 13 na
waombaji uongozi wa Makamu wa Rais na Rais wa TFF watasailiwa tarehe 02
Februari 2013 kuanzia saa 4 asubuhi.
Vyombo vingi vya habari
vimeonyesha nia ya kuwepo mdahalo wa wagombea uongozi katika TPL Board na TFF.
Kanuni za Uchaguzi za TFF hazizuii jambo hilo kufanyika, bali tu lizingatie
Kanuni za Uchaguzi za TFF. Mojawapo ya mambo ya kuzingatiwa ni kwamba mdahalo
huo ufanyike wakati wa kipindi cha Kampeni na usiwe na taswira ya kuwapendelea
au kuwabagua baadhi ya wagombea. Kanuni hazimlazimishi mgombea kushiriki
mdahalo.
Pia ni vema mdahalo
ukaandaliwa na kuratibiwa na Taasisi inayounganisha vyombo vya habari au
waandishi wa habari kama TASWA. Kamati ya Uchaguzi ya TFF lazima ijulishwe kwa
maandishi nia hiyo ya kufanyika mdahalo na utaratibu utakaotumika mapema kabla
ya kufanyika mdahalo huo ili kujiridhisha kuwa utaratibu utakaotumika kuandaa
na kuendesha mdahalo haukiuki kanuni za Uchaguzi za TFF.
Kamati ya Uchaguzi ya
TFF inavishukuru vyombo vya habari kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi hadi sasa
na kuwaomba waendelee kufanya hivyo hadi mwisho wa mchakato wa uchaguzi.
No comments:
Post a Comment