Rais wa TFF anayemaliza muda wake, Leodgar Tenga
SIWEZI KUVUMILIA
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KENGELE ya Uchaguzi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF),
imegongwa huku wanamichezo wasiopungua 50 kujitokeza katika kuchukua fomu za
uchaguzi huo.
Ni matunda mazuri kuona wanamichezo wanajitokeza kwa wingi
kuwania nafasi mbalimbali, kama vile Urais, Makamu wa Rais bila kusahau
wajumbe.
Inapendeza mno, maana katika Uchaguzi huo, yap0 majina
ambayo kwa sababu moja ama nyingine yanaleta mvuto na mguso kwa wadau wa
michezo.
Ingawa nafasi ya urais wa TFF wamejitokeza wanamichezo
wanne, akiwamo Jamal Malinzi, Athumani Nyamlani, Omari Nkwarulo na Richard
Rukambura, lakini vita kali ya nafasi hiyo ipo kwa Nyamlani na mwenzake
Malinzi.
Hata hivyo haitoshi, bado upo mguso kutoka kwa Michael
Wambura, Ramadhan Nassib ambao hawa wamejitokeza kuwania nafasi ya Makamu wa
Rais, wakiwa sanjari na Wallace Karia.
Ukiacha nafasi hizo, wanamichezo wengine wamejitokeza
kuwania nafasi za ujumbe, jambo ambalo siachi kulipongeza katika mwelekeo huo
wa uchaguzi wa TFF.
Pamoja na hayo, akili yangu inaanza kuniuma hasa nikiamini
kuwa katika chaguzi nyingi za TFF kumekuwa na kasumba za aina yake. Baaadhi yao
wamekuwa wakifanya mambo kinyume, hivyo kusababisha maabishano au picha mbaya.
Katika kulisema hilo, naamini kanuni za uchaguzi zitafuatwa
bila kupindisha popote ili iwe njia nzuri za kupata viongozi wapya, maana hilo
ndilo lengo la kuhakikisha soka linapiga hatua.
Nasema hilo huku nikiamini kuwa ndio dhumuni kubwa
lililowekwa na Rais anayemaliza muda wake, Leodgar Tenga, ambaye licha ya kuwa
na nguvu kubwa katika sekta ya michezo, lakini alitangaza kutoendelea na nafasi
yake hiyo kwa ajili ya kupisha watu wengine.
Hii ni njia nzuri na kila mmoja anapaswa kuifurahia kwa
namna moja ama nyingine, huku nikishindwa kuvumilia kama kutakuwa na watu wenye
dhamira tofauti.
Uchaguzi wa TFF ulete safu nzuri yenye mipango ya kweli
katika kuinua kiwango cha soka letu na sio kuwaingiza watu ambao hawapo makini.
Na kama hiyo haitoshi, hao wenye uwezo wa kuongoza TFF
wapatikane kutokana na mifumo halali iliyowekwa kwa kupitia Kamati ya Uchaguzi
na nyinginezo ndani ya Shirikisho hilo.
Najua katika Uchaguzi wowote lazima kuwe na patashika au
kutoelewana kwa baadhi ya mambo. Lakini, naamini hayo yataangaliwa kwa umakini
kwa kufuata kanuzi zilizowekwa.
Huo ndio ukweli, huku nikiamini wanamichezo hao, bila
kuangaliwa dini zao, makabila yao au maeneo wanapotoka, watachaguliwa kwa
kuangaliwa uwezo wao wa kuongoza.
Naamini wote wana dhamira ya kweli ya kuendeleza soka letu,
hivyo lolote litakalotokea liwe la kweli na sio kupangwa na wachache wasiokuwa
na nia njema kwa Taifa lao.
Ukiacha Geofrey Kaburu aliyekuwa anaitaka nafasi ya Ujumbe
wa Kamati ya Utendaji ambaye hakurudisha fomu hiyo pamoja na Shufaa Jumanne,
wengine wote wamerudisha fomu zao.
Wanamichezo hao ni Abdallah Mussa, Salum Chama na Kaliro
Samson Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Richard Rukambura, Samuel Nyalla, Titus
Osoro na Vedastus Lufano, Epaphra Swai na Mbasha Matutu, Charles Mugondo, Elly
Mbise na Omari Walii, Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo Ayubu Nyaulingo, Blassy
Kiondo, Nazarius Kilungeja, Selemani Kameya, James Mhagama na Stanley Lugenge.
Wengine ni Athuman Kambi, Francis Ndulane na Zafarani
Damoder, Hussein Mwamba na Stewart Masima, Farid Nahdi, Hassan Othman Hassanoo,
Riziki Majala na Twahili Njoki, David Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud Mvella na
John Kiteve, Davis Mosha, Khalid Mohamed na Kusiaga Kiata, Alex Kamuzelya, Juma
Pinto, Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda.
Wote hawa ni Watanzania wenzetu na wana haki ya kuongoza
nafasi walizoomba, ingawa utaratibu ni kwamba wote hawawezi kupitishwa, hivyo
lazima mchakato uwe wazi katika kuelekea kupatikana viongozi sahihi na wenye
mtazamo wa mpira wa miguu.
kambimbwana@yahoo.com
0712 053949
0753 806087
No comments:
Post a Comment