Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya na mchekeshaji hapa nchini, Mussa Kitale,
amerithi mikoba ya marehemu Hussein Mkiety, Sharomillionea.
Hiyo inatokana na kutesa katika
tasnia hiyo, huku macho na masikio ya watu yakielekezwa kwa kijana huyo kila
anapokuwapo.
Kitale amekuwa nyota na kupendwa
na watu wengi, huku njiani akipita watu kuacha kazi zao na kuanza kumzungumzia
yeye, bila kusahau watoto wanaomuunganishia kwa kuanza kumcheka au kumsalimu.
Katika msiba wa Juma Kilowoko,
Sajuki, msanii huyo aliongoza kwa kuonwa na watu wengi, wakiwamo watoto ambao
muda mwingi walikuwa na shangwe naye.
Kitale alikuwa ndio swahiba mkubwa
wa marehemu Sharomillionea, huku msiba huo ukimchoma na kujikuta mara kwa mara
akilia, kila akiukumbuka msiba wa msanii huyo aliyefia kijijini kwao Lusanga na
kuzikwa huko huko kwa ajali ya gari.
Aina yake kubwa ya uchekeshaji ni
kuuvaa uhusika wa uteja na kupeleka ujumbe wake kwa hadhira.
No comments:
Post a Comment