MCHUNGAJI
Daniel na Hoyce Mbowe, pichani, wanapenda kuwakaribisha wote wanaoongea Kiswahili hapa
Ujerumani na marafiki wengine katika ibada ya pili ya Kiswahili itakayofanyika
Jumapili ya Januari 13 mwaka mwaka huu.
Muda wa
Ibada ni saa saba mchana (13:00 hours) hadi saa tisa mchana ( 15:00 hours),
huku mahali kwa ibada hiyo ni Evangelischen Friedenskirchengemeinde Bonn na
anuani ni Franz-Bücheler-Straße 10. 53129
Bonn
Ibada ya
Kiswahili itakuwa ikifanyika kila Jumapili ya pili ya kila mwezi, ibada ya
Kwanza ilifanyika tarehe 9 mwezi uliopita na kuhudhuriwa na watu wengi.
Mawasiliano:
dmbowe@hotmail.com or hoycembowe@hotmail.com
No comments:
Post a Comment