Pages

Pages

Saturday, January 19, 2013

Extra Bongo kuwatunuku mashabiki kuanzia leo


Ally Choki
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya Extra Bongo, inafanya onyesho la Wiki Nne za Zawadi kwa wale watakaoweza kucheza mtindo wa Kizigo, wakiwa na bendi ya Extra Bongo Next Level, itakayoanza leo Jumamosi, katika Ukumbi wa Meeda, uliopo Sinza, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Handeni Kwetu, Mkurugenzi wa bendi hiyo, Ally Choki, alisema kuwa tuzo hiyo itakuwa ni fedha taslimu Sh 150,000 kwa mshindi wa kwanza, wapili Sh 100,000 na watatu Sh 50,000.

Alisema, kwa kuanzia bendi hiyo itaanza kuwapa tuzo mashabiki wake watakaohudhuria katika onyesho lao la Jumamosi katika Ukumbi wao wa nyumbani Meeda, Sinza jijini Dar es Salaam.

“Mtindo wa Kizigo umekuwa gumzo kwa mashabiki wao wanohudhuria manoyesho yao hivyo wameamua kuwapa jukumu la wao kushindana kuicheza ambapo mshindi atalambishwa kitita hicho cha fedha kama motisha.

“Tuzo hiyo itaendelea katika kumbi mbalimbali za burudani ambazo wanafanya maonyesho yao na watatangaza wiki ijayo itatolewa wapi," alisema.
Aliwataka mashabiki na wapenzi wa bendi hiyo kujitokeza katika onyesho hilo ili kujinyakulia tuzo hiyo yenye lengo pia la kuwaweka karibu na bendi hiyo.
Alifafanua mashabiki watakaohudhuria onyesho watapata burudani ya nyimbo kama 'Fikiri Madinda', 'Maisha Taiti', 'Double Double' na 'Regina Zanzibar', 'Nguzo Tano za Mapenzi',' 'Mtenda Akitendewa'

No comments:

Post a Comment