Yusuphed Mhandeni, pichani
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MCHUMI wa Kata ya Makumbusho wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Yusuph Shaban, maarufu kama (Yusuphed Mhandeni), amewataka viongozi na wadau
kuweka mkazo kwenye suala la michezo, maana linaweza kuleta maendeleo.
Yusuphed aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, ikiwa ni
mipango ya kuwazindua watendaji hasa wa kwenye kata yao ili wawekeze kwenye
michezo na kuwapa fursa vijana kuonyesha uwezo wao uwanjani.
Akizungumza zaidi, Yusuphed ambaye pia ni kada wa CCM katika
Kata ya Makumbusho, alisema kwa kuangalia fani ya michezo, ukiwamo mpira wa
miguu, ngumi na mingineyo, vijana wao watapata ajira.
Alisema hali hiyo inasababisha mkazo kuwekwa humo, hasa kwa
viongozi ambao wana nafasi na sababu zote za kuwapatia watu wao ajira kwa
kupitia michezo.
"Sisi wote kwa pamoja tukiwekeza kwenye michezo, ajira
zitakuwa nyingi, hivyo nadhani watendaji na viongozi kwa pamoja waliangalie
hilo.
"Kwa mfano kata ya Makumbusho ina vijana wengi na wenye
uwezo wa kuingia kwa wingi kwenye michezo, hivyo watu wajuwe wajibu wao,"
alisema Yusuphed.
Mbali na kupenda michezo, Yusuphed ni miongoni mwa wadau
muhimu wa muziki, huku akijitolea kusaidia kwa karibu watu waliokuwa kwenye
sanaa hiyo, wakiwamo wanamuziki.
No comments:
Post a Comment