Maxmilian Bushoke akiwa na mtoto wake Bushoke nyuma.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa siku nyingi nchini, Maxmilian Bushoke,
anatarajia kutambulishwa rasmi katika kikosi cha wanamuziki wa bendi ya
Orchestra Mlimani Park, baada ya kurejea nchini hivi karibuni na kujiunga na
bendi hiyo.
Bushoke alikuwa akiimbia bendi hiyo tangu miaka ya kati ya
1980, kabla ya kuhamia nchini Afrika Kusini alikokuwa akifanya shughuli za
utangazaji.
Akizungunza na Handeni Kwetu jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi
wa Habari na Mawasiliano wa bendi hiyo, Jimmy Chika, alisema Bushoke
atatambulishwa katika Ukumbi wa Pentagon, uliopo Kurasini ambapo pia atafanya
shoo na wanamuziki wenzake kuanzia Jumapili ya Januari 20.
Mwimbaji huyo na mtunzi aliwahi kujizolea sifa baada ya
kutunga nyimbo kama Kiu ya Jibu, Penzi kile cha fikara na nyingine kadhaa.
Bushoke ambaye ni baba mzazi wa msanii wa kizazi kipya, Luta
Bushoke, amekuwa akijiunga na bendi hiyo mara kwa mara alipokuwa akirejea hapa
nchini, ambapo hata hivyo sasa atakuwa na bendi hiyo kwa kipindi kirefu.
No comments:
Post a Comment