Pages

Pages

Wednesday, December 05, 2012

Wazee wa Ngwasuma kukamua Moshi Alhamisi



Nyosh El Sadaat, kiongozi wa Wazee wa Ngwasuma
 
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya muziki wa dansi ya FM Academia, maarufu kama Wazee wa Ngwasuma, Alhamisi hii inatarajia kufanya onyesho la nguvu katika Ukumbi wa Aventure, uliopo mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Kufanyika kwa shoo hiyo katika mji wa Moshi ni mipango ya bendi hiyo kuwapatia burudani mashabiki wao, ukizingatia kuwa muda mrefu wanaishi Dar es Salaam, hivyo kuwabagua wadau wao wengine.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa bendi hiyo, Kelvin Mkinga, alisema kwamba mashabiki wao wa Moshi wajiandae kupata vitu adimu kutoka kwa vijana wake wenye uwezo wa hali ya juu.

Alisema kwamba wanamuziki wao wamejipanga kuhakikisha kuwa mashabiki wao wanapata kitu adimu kutoka kwao, hivyo waende kwa wingi kuangalia kazi nzuri za vijana wao.

“Tunafanya shoo ya nguvu katika ukumbi huo ambao naamini tutawaacha watu katika shangwe za aina yake, ukizingatia kuwa tuna vyimbo nzuri na utundu wa kuimba kwa kiwango cha juu na jinsi ya kuwapa raha mashabiki wetu.

“Waje kwa wingi kujionea jinsi Wazee wa Ngwasuma wanavyofanya mapinduzi katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini, bila kuangalia ushindani uliopo na wale tunaoshindana nao kila siku ya Mungu,” alisema Mkinga.

Bendi hiyo ipo chini ya Rais wa Vijana, Nyosh El Saadat, akiwa na waimbaji wengine mahiri, akiwamo Patchou Mwamba anayewika pia katika tasnia ya filamu hapa nchini.

No comments:

Post a Comment