Pages

Pages

Saturday, December 15, 2012

USHAURI WA BURE



Ingekuwaje Samatta wangekuwa wengi zaidi?
Mbwana Samatta

ETI jamani? Hivi ingekuwaje kama Taifa letu lingekuwa na wachezaji wa soka wanaokipiga nje kama Mbwana Samatta? Wenye njaa ya mafanikio kama yeye? Kwa nafasi tofauti tofauti kama mchezaji huyo aliyeibukia hivi karibuni?

Sijui kama tusingeweza kucheza Kombe la Dunia. Kwanini nasema hivyo, jamaa anacheza soka la uhakika na kuona kweli ni hodari. Hata timu yake ya TP Mazembe inakubali uwezo wake ndio maana kila wakati yupo uwanjani.

Kwa kujua hilo, nadhani wachezaji wengine wa Tanzania wanapaswa kuwa na wivu wa maendeleo na kukazana zaidi na zaidi kwa ajili ya maisha yao. Sisi tunawaombea dua ili muwe wengi zaidi kwa ajili ya mafanikio yenu.

Mhakikishe mnapangilia mlo wenu, kufanya mazoezi ya nguvu, maana soka sio lele mama. Naamini hilo likifanikiwa, mashabiki na Watanzania watafurahia saana.

Anzeni leo basi, wenzenu tumemisi kuwaona kwenye kideo mkipepetana na nyota wengine majuu, akiwamo Didier Drogba, Samuel Eto’o, Theo Walcot, Lionel Mess na wengineo.
Ndio hivyo bwana. Kwani wao waweze wana nini na nyinyi mshindwe mna nini?

No comments:

Post a Comment