Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MAANDALIZI la
pambano la Francis Cheka na bondia Chiotka Chimwemwe toka Malawi litakalochezwa
Desemba 26 mwaka huu kwenye uwanja wa Sheikh Abeid Amani Karume jijini Arusha
yamekamilika.
Fransic Cheka akipima uzito.
Akizungumza mapema leo asubuhi jijini Dar es Salaam, promota wa pambano hilo
hilo, Andrew George amesema taratibu za mchezo huo umekamilika.
"Taratibu zote
za pambano zimekamilika kwa asilimia 90 ikiwa pamoja na kumtumia tiketi bondia
Chiotka Chimwemwe", alisema George.
George alisema ameamua kulipeka
pambano hilo Arusha kwa kuwa anaamini watu wa Arusha wanapenda ngumi na siku
hiyo ni siku ya sikukuu hivyo watakuja kwa wingi pamoja na familia zao kwani
pambano litaanza saa nane mchana.
Pia alisema mabondia watapima uzito
siku ya sikukuu ya krismasi jijini Arusha.
Pambano hili litakuwa ni la
raundi 12 na Mmalawi huyu anajigamba atampiga Cheka ndani ya ardhi ya nchi yake
hivyo kuwasihi watanzania kuja kwa wingi kwani hata ulinzi utakuwepo wa kutosha,
alisema
No comments:
Post a Comment